Lugha Nyingine
Rais Xi atembelea watu mjini Beijing kabla ya Mwaka Mpya wa Jadi, atoa salamu kwa Wachina wote (6)
![]() |
| Rais wa China Xi Jinping, akitembelea duka la chapa ya mikate ya jadi ya Daoxiangcun kwenye sehemu ya biashara ya Longfusi katika Eneo la Dongcheng la Beijing, Februari 10, 2026. (Xinhua/Xie Huanchi) |
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping amewatembelea maofisa wa mashinani na wakazi mjini Beijing alipofanya ukaguzi wa siku mbili kuanzia Jumatatu hadi Jumanne, akitoa salamu za Mwaka Mpya wa Jadi kwa watu wa China wa nchini na ng’ambo kabla ya sikukuu hiyo.
Rais Xi, amewatakia afya njema, mafanikio ya kazi, na furaha ya familia. Pia ameitakia nchi ya China amani na ustawi katika Mwaka huo mpya wa Farasi.
Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China, ni sikukuu muhimu zaidi ya jadi kwa Wachina. Sikukuu hiyo ya Mwaka huu itaanzia Tarehe 17 mwezi huu wa Februari.
Siku ya Jumatatu asubuhi, Rais Xi alitembelea eneo maalum la kitaifa la uvumbuzi wa sayansi na teknolojia za upashanaji wa habari katika E-town ya Beijing, ambapo alitazama maonyesho ya mafanikio ya sayansi na teknolojia za AI na mambo ya roboti, na alizungumza na watafiti na wakuu wa kampuni za teknolojia.
Rais Xi alisema amekuwa na " imani zaidi" katika uvumbuzi wa sayansi na teknolojia wa China baada ya kuona yote yaliyooneshwa katika ukaguzi wake.
Jana Jumanne asubuhi, Rais Xi alifika katika eneo moja la makazi mjini Beijing ambalo lilikarabatiwa kuwa lisiwe na vizuizi na linalowafaa watu wenye umri mkubwa katika maisha yao. Alitembelea kantini ya eneo hilo kwa ajili ya wazee akifahamishwa kuhusu huduma za mlo zinazotolewa hapo.
"Kutunza na kusaidia wazee ni jukumu la pamoja la jamii nzima," Rais Xi amesema, akihimiza juhudi za kujenga mazingira bora kwa ajili ya watu wenye umri mkubwa kufurahia miaka ya uzeeni. .
Katika Eneo la Xicheng, Rais Xi pia alitembelea nyumba moja ya utunzaji wa uzeeni , ambapo alitumia muda kukaa pamoja na wazee, akiwatakia afya njema, maisha marefu na furaha ya sikukuu Mwaka Mpya wa Jadi.
Alipofika katika sehemu ya biashara ya Longfusi katika Eneo la Dongcheng, Rais Xi alifahamishwa kuhusu juhudi za maendeleo ya mji katika eneo hilo. Alisimama kwenye duka la chapa ya mikate ya kijadi ya Daoxiangcun, ambapo alitazama mchakato wa utengenezaji keki.
Kwenye soko la Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi, alitembelea vibanda mbalimbali vinavyouza bidhaa za sherehe na kuzungumza na watu hapo, akieleza kumbukumbu za kutembelea kwake katika eneo hilo alipokuwa kijana. Pia alinunua vyakula maalum na bidhaa za kitamaduni.
Wakati wa ukaguzi wake, Rais Xi alisikiliza ripoti ya kazi kutoka kwa mamlaka za mji wa Beijing na akisifu maendeleo yaliyopatikana katika kazi mbalimbali mjini Beijing.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




