Habari Picha ya Timu ya Doria ya Ndege Hondohondo katika Mkoa wa Yunnan, China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 11, 2026
Habari Picha ya Timu ya Doria ya Ndege Hondohondo katika Mkoa wa Yunnan, China
Wanakijiji wakifahamishwa kuhusu ujuzi wa ndege hondohondo katika Kijiji cha Shiti cha Wilaya ya Yingjiang, Mkoa wa Yunnan, kusini magharibi mwa China, Februari 5, 2026. (Xinhua/Gao Yongwei)

Katika hifadhi ya mazingira ya asili ya Tongbiguan ya Mkoa wa Yunnan, kusini magharibi mwa China, ndege hondohondo, spishi iliyo chini ya ulinzi wa daraja la kwanza nchini China, wako katika kipindi muhimu cha maandalizi ya kuzaliana. Watu wa "Timu ya Doria ya Hondohondo" wanafanya doria kila baada ya muda uliowekwa ili kuhakikisha usalama wao wakati wa kipindi hiki cha kuzaliana.

"Timu hiyo ya Doria ya Hondohondo" iliundwa na wanakijiji wenyeji na walinzi wa misitu. Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2021, watu wa timu hiyo wameongezwa na kufikia 26. Mbali na kufanya doria, wengi wao pia hufanya kazi kama waongoza watalii wa kutazama ndege au wanashiriki katika shughuli za ikolojia, wamezifanya kazi za uhifadhi wa mazingira ya asili na maendeleo ya jamii zifikie hali ya kuenda sambamba.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha