Lugha Nyingine
Jumba la Makumbusho ya Lin Huiyin kufunguliwa kwa majaribio (5)
![]() |
Jumba la Makumbusho ya Lin Huiyin lililoko kwenye Mtaa wa Sanfangqixiang mjini Fuzhou, China litafunguliwa kwa majaribio tarehe 13 mwezi huu.
Li Huiyin ni mzaliwa wa Mkoa wa Fujian. Alikuwa mtaalamu wa ujenzi mwanamke wa kwanza wa China mpya, ambaye pia ni mmoja kati ya wasanifu wa nembo ya taifa ya Jamhuri ya Watu wa China na mpango wa kuboresha Mnara wa Mashujaa wa Umma. Alikuwa mlinzi wa majengo ya kale ya China na mali za urithi wa utamaduni za China kama vile sanaa za Cloisonne.
Mtaa wa Sanfangqixiang ni mahali walipoishi wazazi wa Lin, na pia ni chanzo cha kumbukumbu zake kuhusu maskani yake. Jumba hilo la makumbusho litaonesha nyaraka, vitu halisi na video nyingi zenye thamani kubwa, ili kuwaelezea watazamaji maisha yote ya mlinzi huyu wa mali za urithi wa utamaduni, mafanikio yake ya taaluma, mchango uliotolewa naye katika mambo ya utamaduni pamoja na moyo wake wa uzalendo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




