ChinaVumbuzi | Mpango wa utafiti wa sayari ya mwezi wa China wafanikiwa kupita majaribio ya roketi na chombo kipya cha anga ya juu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 12, 2026
ChinaVumbuzi | Mpango wa utafiti wa sayari ya mwezi wa China wafanikiwa kupita majaribio ya roketi na chombo kipya cha anga ya juu
Picha hii iliyopigwa Februari 11, 2026 ikionyesha chombo cha kurudia kwa wanaanga cha Chombo cha Mengzhou cha anga ya juu cha kizazi kipya cha China kikiwa kwenye eneo la bahari lililopangwa katika majaribio ya usafiri . (Xinhua/Yang Guanyu)

WENCHANG - China imefanikiwa kufanya majaribio ya usafiri wa roketi ya kubeba vyombo ya Changzheng No.10 kwa uthibitishaji wa vielelezo kwenye anga ya chini pamoja na majaribio ya wanaanga kujiokoa wakati wa usafiri unapokabiliwa na shinikizo la hali ya juu kwenye chombo cha Mengzhou cha kubeba wanaanga kwenda anga ya juu.

Shirika la Safari ya Anga ya Juu la China (CMSA) limesema majaribio hayo yaliyofanyika kwenye Eneo la Kurushia Vyombo kwenda Anga ya Juu la Wenchang katika mkoa wa Hainan, yameonyesha mafanikio makubwa katika mpango wa China wa kupeleka wanaanga kwenda anga ya juu kufanya utafiti wa sayari ya Mwezi.

China inalenga kupeleka wanaanga wake kwenye sayari ya mwezi kabla ya 2030. Mengzhou, maana yake ya Kichina ni "chombo cha ndoto", kimeundwa hasa kwa ajili ya jukumu hilo.

Roketi ya Changzheng No.10 ilirushwa saa 5:00 asubuhi (Saa za Beijing). Baada ya kufikia shinikizo la juu la nguvu, chombo hicho cha Mengzhou kilipokea amri kutoka kwenye roketi na kutekeleza kwa mafanikio kutenganisha na kufutwa.

Hatua ya kwanza ya roketi na chombo cha kurudia kwa wanaanga cha chombo cha anga ya juu vilianguka kwa kutengana kwenye maeneo ya bahari chini ya udhibiti kwa mpango uliowekwa.

CMSA imesema majaribio hayo ya jana Jumatano yameonesha mvuto mpya mbalimbali , ikiwa ni pamoja na modeli mpya ya roketi, modeli mpya ya chombo cha anga ya juu na mfumo mpya wa kurushia, vilevile kuhusisha kazi za uokoaji wa baharini.

CMSA imesema kwamba mafanikio ya majaribio hayo yametoa data muhimu ya usafiri wa chombo na uzoefu wa uhandisi kwa ajili ya kupeleka wanaanga kufanya utafiti wa sayari ya mwezi.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha