Lugha Nyingine
Roketi ya kibiashara SD-3 ya China yarusha satalaiti 7 kutoka baharini (2)
YANGJIANG, Guangdong - China imerusha roketi ya kubeba satalaiti ya Smart Dragon-3 (SD-3) Alhamisi kutoka baharini, na kutuma satalaiti saba katika obiti zilizopangwa kwenye anga ya juu.
Roketi hiyo ilirushwa majira ya saa 2:37 mchana kwa saa za Beijing) kutoka baharini karibu na pwani ya Yangjiang, Mkoa wa Guangdong. Miongoni mwa satalaiti hizo saba ni PRSC-EO2 ya Pakistan.
Urushaji huo wa satalaiti wa Alhamisi ni mafanikio muhimu ya ushirikiano wa anga ya juu kati ya China na Pakistan. Satalaiti ya PRSC-EO2 imewekwa vifaa vya macho na taswira zenye ubora wa hali ya juu. Data za kuhisi kwa mbali zitakazopatikana zitaisaidia Pakistan katika nyanja mbalimbali kama vile uchoraji ramani wa ardhi, ufuatiliaji wa mazingira na majanga ya asili, na ulinzi wa maliasili.
Hii ni mara ya nne kwa roketi ya SD-3 kufanya jukumu la kibiashara la kurusha roketi ikiwa na satalaiti kadhaa ndani yake, ikionyesha nguvu zake bora katika kubadilika kulingana na uwezo wa mifumo iliyofungwa, mazingira ya matumizi na uwezo wa huduma za kibiashara.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




