Rais Xi Jinping wa China ampongeza Kim Jong-un kwa kuteuliwa tena kuwa katibu mkuu wa WPK

(CRI Online) Februari 24, 2026

Rais Xi Jinping wa China amemtumia Kim Jong-un salamu za pongezi kwa kuchaguliwa tena kuwa katibu mkuu wa Chama cha Workers cha Korea (WPK) cha Jamhuri ya Watu ya Kidemokrasia ya Korea (DPRK) kwenye Mkutano Mkuu wa tisa wa chama hicho. 

Rais Xi katika pongezi zake hizo za jana Jumatatu amesema China na DPRK ni majirani marafiki wa kijamaa. Amesisitiza kwamba kudumisha, kuimarisha na kuendeleza uhusiano kati ya nchi hizo mbili ni sera isiyoyumbayumba ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na serikali ya China.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha