Meya wa Jiji la New York atoa amri ya marufuku ya kusafiri kutokana na uwepo wa dhoruba

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 24, 2026

Stesheni ya subway ikionekana huku ikiwa na theluji jijini New York, Marekani, Februari 22, 2026. (Xinhua/Zhang Fengguo)

Stesheni ya subway ikionekana huku ikiwa na theluji jijini New York, Marekani, Februari 22, 2026. (Xinhua/Zhang Fengguo)

NEW YORK - Meya wa Jiji la New York (NYC) nchini Marekani Zohran Mamdani siku ya Jumapili alitangaza hali ya hatari na kutoa amri ya marufuku ya kusafiri kutokana na dhoruba ya majira ya baridi kukumba eneo hilo, ikisababisha mamia ya safari za ndege kufutwa.

Marufuku hiyo ya kusafiri ilianza kutekelezwa kuanzia saa 3 usiku (0200 GMT) Jumapili hadi saa 6 mchana (1700 GMT) jana Jumatatu. Jimbo jirani la New Jersey pia lilitoa marufuku ya kusafiri, likizuia magari barabarani, madarajani na kwenye barabara kuu.

Hali ya dharura imetetekezwa katika New York, New Jersey na Connecticut huku dhoruba hiyo ikienea kaskazini mashariki mwa Marekani.

Utabiri mpya wa hali ya hewa unatabiri inchi 12-18 za theluji na upepo wa kasi ya hadi 55 mph kwa Jiji la New York, na kuifanya kuwa moja ya dhoruba kali zaidi za majira ya baridi ambazo jiji hilo limewahi kupitia kwa miaka mingi, vyombo vya habari vya Marekani vimeripoti.

Takwimu kutoka kampuni ya huduma ya ufuatiliaji wa safari za ndege, FlightAware zinaonyesha kwamba theluthi mbili ya safari za ndege zinazoingia na safari 302 za ndege zinazoondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa John F. Kennedy zimefutwa, huku safari 95 zikichelewa.

Katika Uwanja wa Ndege wa LaGuardia, safari 243 za ndege zimefutwa na 122 zikicheleweshwa, wakati huohuo Uwanja wa Ndege wa Newark katika Mji wa New Jersey umeshuhudia kufutwa kwa safari 195 na kucheleweshwa kwa safari 106.

Watu wakitembea kwenye theluji barabarani jijini New York, Marekani, Februari 22, 2026. (Xinhua/Zhang Fengguo)

Watu wakitembea kwenye theluji barabarani jijini New York, Marekani, Februari 22, 2026. (Xinhua/Zhang Fengguo)

Magari yakiendeshwa kwenye theluji barabarani jijini New York, Marekani, Februari 22, 2026. (Xinhua/Zhang Fengguo)

Magari yakiendeshwa kwenye theluji barabarani jijini New York, Marekani, Februari 22, 2026. (Xinhua/Zhang Fengguo)

Watu wakitembea kwenye theluji katika stesheni ya subway jijini New York, Marekani, Februari 22, 2026. (Xinhua/Zhang Fengguo)

Watu wakitembea kwenye theluji katika stesheni ya subway jijini New York, Marekani, Februari 22, 2026. (Xinhua/Zhang Fengguo)

Barabara kuu iliyofungwa ikionekana huku ikiwa na theluji jijini New York, Marekani, Februari 22, 2026. (Xinhua/Zhang Fengguo)

Barabara kuu iliyofungwa ikionekana huku ikiwa na theluji jijini New York, Marekani, Februari 22, 2026. (Xinhua/Zhang Fengguo)

Watu wakitembea kwenye theluji katika eneo la Times Square jijini New York, Marekani, Februari 22, 2026. (Xinhua/Zhang Fengguo)

Watu wakitembea kwenye theluji katika eneo la Times Square jijini New York, Marekani, Februari 22, 2026. (Xinhua/Zhang Fengguo)

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Renato Lu)

Picha