Waziri Mkuu wa Tanzania ahimiza taasisi ya sayansi ya Nelson Mandela kutoa kipaumbele kwa uvumbuzi

(CRI Online) Februari 24, 2026

Waziri Mkuu wa Tanzania Bw. Mwigulu Nchemba, ameihimiza taasisi ya Sayansi na Teknolojia Afrika ya Nelson Mandela mkoani Arusha, kubadilika kuwa kitovu cha elimu bora na utafiti wa kisasa unaolenga kutatua changamoto halisi.

Akizungumza kwenye hafla ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa hosteli mpya kwenye kampasi ya Tengeru ya taasisi hiyo, Nchemba ametaja uvumbuzi ulioanzishwa ndani ya nchi kutoka kwenye taasisi hiyo, ikiwa ni pamoja na chanjo za samaki, mbolea za unga wa mwani wa baharini na droni za kilimo kwa ajili ya kupanda mazao, kuwa zinaongeza uzalishaji na kurahisisha maisha ya kila siku.

Ametoa wito kwa taasisi hiyo kutoa kipaumbele kwa ujuzi wa kivitendo, uvumbuzi na ujasiriamali ili wahitimu waweze kujitengenezea fursa za ajira badala ya kutegemea ajira za serikali pekee.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha