Wiki ya Nishati Endelevu ya SADC yafunguliwa Zimbabwe

(CRI Online) Februari 24, 2026

Wiki ya Nishati Endelevu ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) imefunguliwa Jumatatu katika mji wa kitalii wa Victoria Falls nchini Zimbabwe, ikitoa wito wa kuhimiza nishati mbadala na ufanisi wa nishati.

Tukio hilo lenye kaulimbiu ya“Kuchochea Ukuaji wa Uchumi wa Kikanda Kupitia Nishati Safi na Ufanisi wa Nishati”, linawaleta pamoja wadau wa sekta ya nishati, zikiwemo taasisi za kikanda, idara za serikali, sekta binafsi, akademia na washirika wa maendeleo, ili kuimarisha ushirikiano wa kikanda katika sekta hiyo.

Akifungua tukio hilo, Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Umeme wa Zimbabwe July Moyo amesema kuna haja ya kufanya jitihada za pamoja kupanua matumizi ya nishati mbadala katika eneo la Kusini mwa Afrika.

“Tunahitaji kuimarisha mifumo yetu ya usimamizi kupitia kusawazisha sheria, ushuru na matumizi ya mifumo.”amesema.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha