Lugha Nyingine
Tanzania yatafuta kuongeza uhusiano wa kiuchumi na Singapore katika biashara, akili mnemba na utozaji kodi za kidijitali
(CRI Online) Februari 24, 2026
Waziri wa Fedha wa Tanzania Bw. Khamis Mussa Omar amesema Tanzania imedhamiria kuzidisha ushirikiano na Singapore katika sekta muhimu za ukuaji, ikiwa ni pamoja na biashara, uwekezaji, utalii, AI, na mifumo ya mapato ya kidijitali.
Omar, ameyasema hayo mjini Dar es Salaam wakati akizungumza na Balozi wa Singapore nchini Tanzania Bw. Douglas Foo.
Omar amesema pande zote mbili zimekubaliana kuimarisha ushirikiano wa pande mbili katika nyanja za kiuchumi, kijamii na kidiplomasia, huku zikizingatia kuharakisha makubaliano kuhusu ulinzi wa uwekezaji na kuepuka utozaji kodi mara mbili.
Kwa upande wake Balozi Foo amesema Singapore itahimiza kampuni na taasisi zake kuwekeza na kuhamishia teknolojia Tanzania.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



