Lugha Nyingine
Shirika la Habari la Xinhua lachapisha kitabu kuhusu utawala wa China chini ya uongozi wa Rais Xi Jinping

Picha hii ikionyesha matoleo ya lugha ya Kichina na Kiingereza ya juzuu ya kwanza ya Kitabu cha "Utawala wa China Chini ya Uongozi wa Xi Jinping." (Xinhua/Cai Yang)
BEIJING – Shirika la Uchapishaji la Xinhua ambalo ni kitengo cha Shirika la Habari la China, Xinhua, limetoa juzuu ya kwanza ya Kitabu cha "Utawala wa China Chini ya Uongozi wa Xi Jinping", kitabu hicho kimehaririwa na shirika hilo la habari, na kimekuwa na matoleo ya lugha za Kichina na Kiingereza yatakayotolewa kwa wasomaji ndani na nje ya China.
Tokea Mkutano Mkuu wa 18 wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), Kamati Kuu ya Chama ambayo Xi akiwa katibu wake mkuu, kwa juhudi kubwa za kihistoria, ujasiri mkubwa wa kisiasa na ubebaji wa wajibu imepata mafanikio ya kihistoria na kuleta mabadiliko ya kihistoria katika mambo ya Chama na nchi.
Katika uzoefu mkubwa uliofanywa katika zama mpya, Fikra ya Xi Jinping juu ya ujamaa wenye umaalum wa China wa zama mpya imeundwa hatua kwa hatua, na kuwa dira ya kisayansi ya vitendo vya kujenga nchi yenye nguvu ya mambo ya kisasa ya kijamaa kwa pande zote, na kuhimiza ustawishaji mkubwa wa Taifa la China.
Waandishi wa habari wa Xinhua wameshuhudia historia kadri inavyojidhihirisha, wakitoa habari nyingi zinazoonesha fikra ya kina, utendaji mpana, kujitolea kithabiti, na mafanikio makubwa ya Xi, katibu mkuu wa Kamati Kuu ya CPC, katika utawala wa nchi.
Juzuu hiyo ya kwanza imekusanya makala simulizi 26 za Xinhua na habari picha 41 za Xi, ambazo zimeonesha uongozi wake wenye maono katika kuiongoza China kuelekea ustawishaji wa taifa, na nguvu kubwa ya utendaji ya Fikra ya Xi Jinping juu ya Ujamaa wenye Umaalum wa China wa Zama Mpya.
Kongamano kuhusu usimamizi wa Dunia na hafla ya kutolewa kwa vitabu vya toleo la Kiingereza imefanyika jana Jumanne mjini Geneva, Uswizi. Wageni walioshiriki kwenye shughuli hiyo wamesifu sana utafutaji na fikra za China katika kazi ya utawala wa nchi wa zama mpya, na wameonyesha nia yao ya kuongeza zaidi mawasiliano na ushirikiano na China katika nyanja ya usimamizi wa Dunia.

Picha hii ikionyesha toleo la lugha ya Kichina la juzuu ya kwanza ya Kitabu cha "Utawala wa China Chini ya Uongozi wa Xi Jinping." (Xinhua/Cai Yang)

Picha hii ikionyesha toleo la lugha ya Kiingereza la juzuu ya kwanza ya Kitabu cha "Utawala wa China Chini ya Uongozi wa Xi Jinping." (Xinhua/Cai Yang)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



