China kuendelea na juhudi chanya katika kuhimiza utatuzi wa kisiasa kwa mgogoro wa Ukraine

(CRI Online) Februari 25, 2026

Konsuli wa Ujumbe wa Kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Teng Fei amesema kuwa katika kipindi hiki muhimu, China inatarajia jumuiya ya kimataifa kuweka mazingira wezeshi kwa ajili ya kuhimiza utatuzi wa kisiasa kwa mgogoro wa Ukraine, na inatarajia kuwa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa litafanya kazi ya kiujenzi katika kuleta maafikiano juu ya amani miongoni mwa nchi wanachama.

Balozi Teng ameyasema hayo katika maelezo yake kufuatia kura ya azimio la "Kuunga mkono Amani ya Kudumu nchini Ukraine" kwenye kikao maalum cha dharura cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kilichofanyika jana Jumanne ambapo amesema, China pia itaendelea na juhudi za kuhimiza utatuzi wa kisiasa kwenye mgogoro huo.

Ameongeza kuwa China inahimiza na kuunga mkono juhudi zote zinazofanywa kwa ajili ya amani, na inatoa wito kwa pande zote zinazohusika kudumisha mwelekeo chanya, kuendelea kujenga maoni ya pamoja, na kujitahidi kufikia makubaliano ya amani yaliyo kamili, ya kudumu, na yenye nguvu za kisheria.

“Ni muhimu kushughulikia mizizi ya chanzo cha matatizo ili kuunda mfumo wa usalama wa Ulaya ulio na uwiano, wenye ufanisi, na endelevu zaidi na hivyo kufikia amani na utulivu wa kudumu barani Ulaya.” amesema.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha