Iran yasisitiza nia ya kufikia makubaliano ya nyuklia huku Marekani ikituma ndege zaidi za kivita

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 25, 2026

Picha hii iliyopigwa Februari 20, 2026 ikionyesha mandhari ya jiji la Tehran, Iran. (Xinhua/Shadati)

Picha hii iliyopigwa Februari 20, 2026 ikionyesha mandhari ya jiji la Tehran, Iran. (Xinhua/Shadati)

CAIRO - Maafisa waandamizi wa Iran wamesisitiza nia ya Iran kufikia makubaliano ya nyuklia na Marekani, huku Washington ikiendelea kuongeza uwepo wake wa kijeshi katika eneo la Mashariki ya Kati, ikituma ndege za kivita za teknolojia ya hali ya juu.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Seyed Abbas Araghchi amesema Jumanne kuwa Iran imeazimia kufikia makubaliano "ya haki na usawa" na Marekani mapema iwezekanavyo.

Katika maelezo yake yaliyochapishwa kwenye mtandao wa X, Araghchi amesema pande hizo mbili zina "fursa ya kihistoria" ya kufikia makubaliano ambayo hayajawahi kutokea ambayo yanashughulikia masuala yanayofuatiliwa ya pande zote mbili na kufikia maslahi ya pamoja, akiongeza kuwa makubaliano yako ndani ya uwezekano kama diplomasia itapewa kipaumbele.

Maoni yake hayo yamekuja kabla ya duru ya tatu ya mazungumzo ya nyuklia yasiyo ya moja kwa moja kati ya Tehran na Washington, yaliyopangwa kufanyika kesho Alhamisi mjini Geneva. Duru mbili za mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja zilifanyika mapema mwezi huu, zikilenga mpango wa nyuklia wa Iran na uwezekano wa kuondolewa kwa vikwazo vya Marekani.

Pia siku hiyo ya Jumanne, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayehusika na Masuala ya Siasa Majid Takht Ravanchi alisema Iran iko tayari kufanya "chochote kinachohitajika" kufikia makubaliano ya nyuklia na Marekani.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Seyed Abbas Araghchi (kulia) akihudhuria mkutano wa pamoja na waandishi wa habari jijini Tehran, Iran, Januari 18, 2026. (Xinhua/Shadati)

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Seyed Abbas Araghchi (kulia) akihudhuria mkutano wa pamoja na waandishi wa habari jijini Tehran, Iran, Januari 18, 2026. (Xinhua/Shadati)

Wakati huo huo, kwenye mkutano jijini Tehran na Waziri wa Ulinzi wa Armenia Suren Papikyan siku hiyo ya Jumanne, Waziri wa Ulinzi wa Iran Aziz Nasirzadeh amesisitiza azma thabiti ya nchi yake ya kujilinda.

Amesema Iran haitafuti vita, "lakini kama vita vitalazimishwa kwa nguvu kwa nchi hiyo, itajilinda kwa nguvu na kutoa somo lisilosahaulika kwa maadui."

Kauli hiyo inafuatia mazoezi ya kijeshi yaliyofanywa na Vikosi vya Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) kwenye pwani ya kusini mwa Iran, shirika la habari la Fars linalomilikiwa kwa sehemu na serikali ya Iran limeripoti Jumanne.

Mazoezi hayo yamefanyika huku kukiwa na kujizatiti kijeshi kwa Marekani kunakoendelea katika eneo la Mashariki ya Kati na vyombo vya habari vinaripoti kwamba Rais wa Marekani Donald Trump alikuwa akifikiria kuanzisha shambulizi la hatua ya kwanza dhidi ya Iran.

Picha hii iliyopigwa Februari 9, 2026 ikionyesha mandhari ya jiji la Tehran, Iran. (Xinhua/Shadati)

Picha hii iliyopigwa Februari 9, 2026 ikionyesha mandhari ya jiji la Tehran, Iran. (Xinhua/Shadati)

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha