Lugha Nyingine
Uganda yapata hisa katika Kampuni ya KPC ya Kenya ili kulinda ugavi wa mafuta
Serikali ya Uganda imeidhinisha kampuni yake ya mafuta inayoendeshwa na serikali kununua asilimia 20.15 ya hisa katika Kampuni ya Kenya Pipeline (KPC) kabla ya mpango wake wa uuzaji wa awali wa sehemu ya hisa zake kwa wawekezaji wa umma (IPO).
Akiongea na wanahabari jana Jumanne Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini wa Uganda Ruth Nankabirwa, amesema Baraza la Mawaziri la nchi hiyo Jumatatu liliidhinisha Kampuni ya Taifa ya Mafuta ya Uganda (UNOC) kushiriki katika mchakato huo wa IPO wa KPC.
Nankabirwa amesema uwekezaji huo ni muhimu kwa sababu kampuni ya UNOC ambayo ni muagizaji pekee wa bidhaa za petroli kutoka nje wa Uganda, inategemea KPC kusafirisha mafuta kutoka bandari ya Mombasa ya Kenya hadi magharibi mwa Kenya, na hatimaye husafirishwa hadi Uganda.
Kwa mujibu wa takwimu rasmi, uagizaji mafuta kupitia Kenya unachangia asilimia zaidi ya 95 ya mahitaji ya mafuta ya mwezi ya Uganda, yaani lita takriban bilioni 2.96 kwa mwaka, huku asilimia 5 iliyobaki ikiingizwa kupitia nchi jirani ya Tanzania.
Kenya inapanga kubinafsisha sehemu ya KPC kwa kuiorodhesha kwenye NSE, ikisaliwa na asilimia 35 ya hisa huku ikitoa asilimia 65 iliyobaki kwa umma.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



