Lugha Nyingine
Botswana na Zambia zazindua Mamlaka ya Daraja la Kazungula ili kupanua biashara ya kikanda
Rais wa Botswana Duma Boko na mwenzake wa Zambia, Hakainde Hichilema, wamezindua rasmi Mamlaka ya Daraja la Kazungula katika kituo cha mpakani kaskazini mwa Botswana jana Jumanne.
Mamlaka hiyo mpya iliyoanzishwa itashughulikia usimamizi wa daraja na kituo chake cha mpakani.
Wakizungumza kwenye hafla ya uzinduzi, viongozi hao wawili wamesema kuanzishwa kwa mamlaka hiyo ni hatua muhimu kuelekea kutumia kikamilifu Daraja la Kazungula ili kupanua biashara ya kikanda na kuongeza tija chini ya Eneo la Biashara Huria la Afrika (AfCFTA), wakitoa wito wa kuongezwa kwa uwekezaji wa pamoja ili kuendeleza maendeleo na biashara kati ya mataifa yao.
Akizungumza katika hafla hiyo, Rais Boko amesema mamlaka hiyo itaimarisha uhusiano wa pande mbili kwa kutengeneza njia muhimu za usafirishaji wa bidhaa na watu.
Kwa upande wake, Rais Hichilema amesisitiza umuhimu wa kuimarisha biashara ya kikanda ya AfCFTA na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) kupitia mipango kama huo wa Daraja la Kazungula.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



