China na Ujerumani zakubaliana kuendeleza kwa kina uhusiano wa washirika na ushirikiano wa kunufaishana

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 26, 2026

Rais wa China Xi Jinping akikutana na Chansela wa Ujerumani Friedrich Merz, ambaye yuko katika ziara rasmi nchini China, kwenye Jumba la Kupokea Wageni wa Kitaifa la Diaoyutai mjiniBeijing, China, Februari 25, 2026. (Xinhua/Li Xiang)

Rais wa China Xi Jinping akikutana na Chansela wa Ujerumani Friedrich Merz, ambaye yuko katika ziara rasmi nchini China, kwenye Jumba la Kupokea Wageni wa Kitaifa la Diaoyutai mjini Beijing, China, Februari 25, 2026. (Xinhua/Li Xiang)

BEIJING - Rais wa China Xi Jinping amekutana na Chansela wa Ujerumani Friedrich Merz mjini Beijing jana Jumatano, ambapo pande zote mbili zimekubaliana kuhimiza maendeleo mapya ya uhusiano wa wenzi wa kimkakati kwa pande zote, kuhimiza mazungumzo na ushirikiano, na kushikilia ushirikiano wa pande nyingi na biashara huria.

Hii ni mara ya kwanza kwa Chansela Merz kufanya ziara nchini China tangu aingie madarakani.

Rais Xi amesema China na Ujerumani ni nchi ya pili na ya tatu kwa ukubwa wa uchumi wao duniani, na uhusiano wa pande hizi mbili si tu unahusiana na maslahi ya nchi hizo mbili, bali pia unaweza kuleta ushawishi muhimu kwa Ulaya na dunia.

"Hali ya muundo wa kimataifa inapitia mabadiliko ya kina zaidi baada ya Vita vya Pili vya Dunia" Rais Xi amesema, akiongeza kuwa kadiri dunia inavyokabiliwa na mabadiliko na misukosuko zaidi, ndivyo maendeleo mapya yanavyoonekana kuwa muhimu zaidi kwa nchi hizo mbili katika kuimarisha mawasiliano ya kimkakati, kuimarisha hali ya kuaminiana kimkakati na kuendeleza uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa pande zote kati ya China na Ujerumani.

Rais Xi amesema nchi zote mbili zinapaswa kuwa washirika wanaotegemeana, kwani China na Ujerumani zote zinatafuta kujiamulia na kupata maendeleo ya haraka. Amesema nchi hizo mbili zimeshikilia kuheshimiana, kuaminiana na kufanya ushirikiano wa kufungua mlango, na kwa pamoja zimeandika simulizi za mafanikio ya ushirikiano wa kunufaishana.

"China inashikilia kufuata njia ya maendeleo ya amani, na ina uwezo na imani kwa kufikia mambo ya kisasa ya aina ya China. China itaendelea kunufaika na fursa za maendeleo pamoja na Ujerumani na nchi nyingine mbalimbali duniani," amesema.

Rais Xi amesema China na Ujerumani zinapaswa kuhifadhi nafasi kuu ya Umoja wa Mataifa, kusisitiza kazi ya uongozi ya Umoja wa Mataifa, na kutangulia mbele katika kulinda ushirikiano wa pande nyingi, kutekeleza sheria za kimataifa, kulinda biashara huria, na kutetea mshikamano na uratibu.

Kwa upande wake Chansela Merz amesema, upande wa Ujerumani unatilia maanani uhusiano wake na China na kushikilia kithabiti sera ya kuwepo kwa China moja, na unapenda kushirikiana na China katika kuendeleza urafiki wa jadi, kuendelea kuheshimiana na kufanya ushirikiano wa kufungua mlango , na kuendeleza kwa kina uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa pande zote.

Rais wa China Xi Jinping akikutana na Chansela wa Ujerumani Friedrich Merz, ambaye yuko katika ziara rasmi nchini China, kwenye Jumba la Kupokea Wageni wa Kitaifa la Diaoyutai mjini Beijing  Februari 25, 2026. (Xinhua/Yin Bogu)

Rais wa China Xi Jinping akikutana na Chansela wa Ujerumani Friedrich Merz, ambaye yuko katika ziara rasmi nchini China, kwenye Jumba la Kupokea Wageni wa Kitaifa la Diaoyutai mjini Beijing Februari 25, 2026. (Xinhua/Yin Bogu)

Chansela Merz amesema sekta ya viwanda vya Ujerumani inatilia maanani sana soko la China, na inatarajia kuzidisha zaidi ushirikiano na China ili kupata matokeo ya kunufaishana na maendeleo kwa pamoja.

Rais wa China Xi Jinping akitembea na Chansela wa Ujerumani Friedrich Merz, ambaye yuko katika ziara rasmi nchini China, baada ya mkutano wao kwenye Jumba la Kupokea Wageni wa Kitaifa la Diaoyutai mjini Beijing, China, Februari 25, 2026. (Xinhua/Shen Hong)

Rais wa China Xi Jinping akitembea na Chansela wa Ujerumani Friedrich Merz, ambaye yuko katika ziara rasmi nchini China, baada ya mkutano wao kwenye Jumba la Kupokea Wageni wa Kitaifa la Diaoyutai mjini Beijing, China, Februari 25, 2026. (Xinhua/Shen Hong)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha