China yatumai Marekani itatazama utekelezaji wa makubaliano ya biashara ya awamu ya kwanza kwa njia ya kimantiki na isiyo na upendeleo

(CRI Online) Februari 26, 2026

Wizara ya Biashara ya China imesema kuwa China inatumai kwamba Marekani itatazama utekelezaji wa makubaliano ya kiuchumi na kibiashara ya awamu ya kwanza kati ya China na Marekani kwa busara na bila upendeleo.

Kauli hiyo ya Wizara ya Biashara ya China imetolewa jana Jumatano kwenye mkutano na waandishi wa habari, wakati wa kujibu swali kwamba Mwakilishi wa Biashara wa Marekani Greer aliripotiwa akisema kuwa Marekani itaendelea kuendeleza uchunguzi wa Kifungu cha 301 kuhusu utekelezaji wa makubaliano hayo ya awamu ya kwanza.

Wizara hiyo imesema kuwa kama Marekani itasisitiza kuendeleza uchunguzi wake huo, au kuutumia kama kisingizio cha kuanzisha hatua za vizuizi kama vile ushuru, China itachukua hatua zote muhimu ili kulinda haki na maslahi yake halali.

Imesema kwamba tangu makubaliano hayo ya kiuchumi na kibiashara ya awamu ya kwanza yaanze kutekelezwa rasmi mapema mwaka 2020, China, ikishikilia moyo wa makubaliano hayo, imejitahidi kushinda athari ya ghafla ya janga la COVID na usumbufu wa mnyororo wa usambazaji, mdororo wa uchumi duniani na mambo mengine yenye athari mbaya yaliyotokana nalo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha