Zimbabwe yasitisha mazungumzo na Marekani juu ya mpango wa ufadhili wa afya

(CRI Online) Februari 26, 2026

Gazeti la serikali ya Zimbabwe, The Herald limeripoti Jumatano kuwa Zimbabwe imesitisha mazungumzo na Marekani juu ya pendekezo la Mkataba wa Makubaliano wa Ufadhili wa Afya (MoU).

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, makubaliano hayo yaliyokuwa yamependekezwa yalikuwa yakitoa ufadhili mkubwa wa afya kwa kubadishana na ufikiaji kamili wa data nyeti za afya za nchi hiyo, zikiwemo za sampuli za vimelea na taarifa za magonjwa kutoka kwa raia wake.

Katika ujumbe wake kwenye mtandao wa X, msemaji wa serikali ya Zimbabwe Nick Mangwana amesema, “tatizo ni kwamba Zimbabwe ilikuwa ikiombwa kutoa rasilimali na data za kibaolojia kwa muda mrefu, bila kuwa na hakikisho la kupata chanjo au matibabu kutokana na matokeo ya rasilimali hizo. Marekani haikutoa majibu sawa ya kuchangia data zake za magonjwa na mamlaka za afya za Zimbabwe.”

“Kimsingi, mpango huo haukuwa wa ulinganifu.” Ujumbe huo umeongeza.

Ubalozi wa Marekani nchini Zimbabwe Jumatano ulitoa taarifa ukisema Marekani haijafurahishwa na uamuzi huo wa serikali ya Zimbabwe.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha