Lugha Nyingine
Tamasha la vyombo vya habari la Afrika lafunguliwa nchini Kenya likitoa wito wa kuimarisha uhimilivu wa sekta
Tamasha la Nne la Vyombo vya Habari la Afrika (AMF) limeanza rasmi jana Jumatano jijini Nairobi, nchini Kenya, likiwaleta pamoja wajumbe zaidi ya 200 kutoka nchi karibu 40 ili kubainisha njia za kiuvumbuzi za kuimarisha uhimilivu wa uchumi bunifu huku kukiwa na teknolojia mpya zinazobadili hali ya sekta hiyo.
Likiandaliwa na Baraza la Media Lab, shirika lisilo la faida lenye makao yake makuu jijini Nairobi, tamasha hilo la 2026 linafanyika chini ya kaulimbiu ya "Uelezeaji Himilivu wa Simulizi: Kufikiria Upya Uhuru wa Vyombo vya Habari".
Washiriki katika tamasha hilo la siku mbili ni pamoja na watunga sera waandamizi, wahariri, waandaji maudhui, wasomi, na wavumbuzi kutoka barani kote wanaojikita katika kuboresha mwonekano wa simulizi za Afrika kupitia majukwaa ya vyombo vya habari vya jadi na vipya.
Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza Media Lab, Daniel Kalinaki amesema kwamba vyombo vya habari vya Afrika vimeonyesha uhimilivu katika kukabiliana na mambo mapya yaliyoletwa na teknolojia mpya, siasa tete za kijiografia, na shinikizo la kifedha, huku kampuni mpya za vyombo vya habari zikichukua jukumu kubwa katika kuunda upya simulizi za bara hilo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



