Mcheza Skating Zhang Dan: Moyo wa Olimpiki Unatufanya Tuwe Wajasiri, Imara na Watulivu Zaidi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 26, 2026

Katika mwaka huu wa 2026, mwenge wa Olimpiki umewashwa tena nchini Italia, ikiashiria kurejea kwa Michezo hiyo ya Majira ya Baridi nchini humo baada ya miaka 20. Katika miongo miwili iliyopita tangu Turin 2006, alama zilizoachwa kwenye barafu kwa muda mrefu zimeweza kufunikwa na magwiji wapya. Hata hivyo, simulizi za michezo hiyo ya 2006 zinaendelea kuishi.

Kuanzia kushindana kwenye Olimpiki miaka 20 iliyopita hadi kumfundisha binti yake kuzungusha mwili na kuruka kwenye barafu leo, Zhang Dan, mcheza skating wa jozi wa zamani wa China, amekuwa akihusiana kwa kina na mchezo wa minyumbuliko ya dansi ya kuteleza kwenye barafu (figure skating). Zhang ni bingwa wa dunia wa mara nyingi na alinyakua medali ya fedha katika mchezo wa minyumbuliko ya dansi ya kuteleza kwenye barafu kwa mtindo huria (Pairs Free Skating) kwenye Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Turin 2006 pamoja na mwenzake, Zhang Hao.

Baada ya kustaafu kutoka kwenye mashindano, Zhang alianzisha kituo cha mafunzo ya mchezo huo kwa vijana na kuwa mhusika mkuu katika maigizo ya kwanza ya minyumbuliko ya dansi kwenye barafu ya China. Binti yake, Qiqi, amerithi kipaji cha mama yake na sasa anajifunza mchezo huo. Kama kocha, Zhang anatumai Qiqi anaweza kupata matokeo bora zaidi; kama mama, anataka binti yake kuwa mstahimilivu na jasiri kupitia mchezo huo.

Zhang amesema kuwa moyo wa Olimpiki kwa muda mrefu umekuwa sehemu ya kila upande wa maisha yake. Kwake yeye, jambo la muhimu zaidi kuliko kuwashinda wengine ni kujishinda mwenyewe wa zamani.

"Tumejitahidi bila kuchoka kwa ndoto zetu, na moyo wa Olimpiki unatuwezesha kuwa wajasiri zaidi, imara zaidi, na watulivu zaidi katika safari ndefu ya maisha," amesema.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha