Rais Xi ahimiza mwanzo mzuri wa kipindi cha Mpango wa 15 wa Miaka Mitano

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 27, 2026

BEIJING – Rais wa China Xi Jinping, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), amewataka maofisa waandamizi wa CPC kuhakikisha mwanzo mzuri wa kipindi cha Mpango wa 15 wa Miaka Mitano (2026-2030).

Xi ameyasema hayo baada ya kusoma ripoti za kazi za mwaka za maofisa waandamizi wa Chama zilizowasilishwa hivi karibuni kwa Kamati Kuu ya CPC na kwake.

Maofisa hao waliowasilisha ripoti zao za kazi ni pamoja na wajumbe wa Ofisi ya Siasa na Ofisi ya Makatibu za Kamati Kuu ya Chama, wajumbe wa vikundi vya uongozi wa Chama vya Bunge la Umma la China, Baraza la Serikali la China, na Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China, pamoja na makatibu wa vikundi vya uongozi wa Chama vya Mahakama Kuu ya Umma ya China na Idara kuu ya Uendeshaji wa Mashtaka ya China.

Rais Xi ametoa wito wa kuwataka maofisa hao siku zote kufuata nidhamu na kanuni, mwelekeo na njia za Kamati Kuu ya Chama katika fikra, msimamo wa kisiasa, na vitendo, na kuchukua hatua halisi kwa kuhakikisha maamuzi na mipango ya Kamati Kuu ya Chama inatekelezwa kwa pande zote.

"Maofisa wa ngazi zote wanapaswa kubeba wajibu kwa hiari katika majukumu yao tofauti mbalimbali, na kutekeleza kwa makini kanuni nane za kuboresha mienendo zilizowekwa na Kamati Kuu ya Chama na vifungu vya utekelezaji wa kanuni hizo," Xi amesema.

Amewahimiza wawe watangulizi wenye mtazamo sahihi na kutekeleza kwa vitendo majukumu yao ya kisiasa, ili kupata mafanikio halisi kwa kupitia juhudi zao kubwa za kufanya kazi kwa ajili ya umma.

"Ni lazima kujenga mazingira safi ya kisiasa iliyo ya kufuata maadili bila ufisadi," Xi amesema.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha