Lugha Nyingine
Marekani yadaiwa kuweka masharti magumu katika mazungumzo na Iran huko Geneva
Kwa mujibu wa habari iliyochapishwa na jarida la Wall Street jana Alhamisi, katika duru mpya ya mazungumzo ya nyuklia ya Geneva kati ya Marekani na Iran, Marekani imetaka makubaliano ambayo ndani yake Iran itabomoa vituo vyake vitatu vya nyuklia na kuhamisha uraniamu yote iliyobaki iliyorutubishwa nchini Marekani.
Habari hiyo ikinukuu maafisa wa Marekani imesema kwamba ikulu ya White House inasisitiza kwamba Iran ifunge shughuli zake kwenye vituo vyake vikuu vya nyuklia vya Fordow, Natanz na Isfahan, ikubali makubaliano bila kikomo cha kuisha muda wake, ikilenga kuzuia kabisa njia ya Iran ya kupata silaha za nyuklia.
Habari hiyo inasema Marekani inasisitiza kutokuwepo kwa urutubishaji wa madini ya uraniamu, lakini timu yake ya mazungumzo inaweza kuruhusu Iran kuanzisha upya mtambo wake wa nyuklia mjini Tehran ambao unaweza kusindika uraniamu iliyorutubishwa kwa kiwango cha chini kwa malengo ya kimatibabu.
Kwa upande wake Iran inasisitiza haki yake ya kurutubisha uraniamu lakini inatafuta kuituliza Marekani kwa mapendekezo iliyoyatoa yanayojumuisha kupunguza urutubishaji hadi hata asilimia 1.5 kutoka asilimia hadi 60, kusimamisha urutubishaji kwa miaka kadhaa, au kuisindika kupitia kampuni ya ubia kati ya nchi ya Kiarabu na Iran yenye makao yake Iran, habari hiyo imesema.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



