Lugha Nyingine
Hillary Clinton atoa ushahidi kwamba "hakujua chochote" kuhusu uhalifu wa Epstein
Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje wa Marekani Hillary Clinton amewaambia wabunge wa Baraza la Wawakilishi la Marekani jana Alhamisi kwamba hakujua chochote kuhusu uhalifu wa Jeffrey Epstein na mwenzake Ghislaine Maxwell.
“Sikujua chochote kuhusu shughuli zao za uhalifu. Sikumbuki kukutana na Bw. Epstein. Sijawahi kupanda ndege pamoja naye au kutembelea kisiwa, nyumba au ofisi zake. Sina jambo lingine la kuongeza katika hilo” amesema kwenye taarifa yake iliyochapishwa kwenye mitandao ya kijamii.
Taarifa hiyo imekuja kabla hajatoa ushahidi wake wa faragha mbele ya Kamati ya Usimamizi na Mageuzi ya Serikali ya Baraza la Wawakilishi huko Chappaqua, New York.
Mumewe, Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton, atakwenda kutoa ushahidi kama huo leo Ijumaa, ambayo itakuwa ni mara ya kwanza kwa rais mstaafu kutoa ushahidi mbele ya Bunge tangu 1983.
Katika taarifa hiyo, Clinton ameishutumu kamati hiyo kwa kujaribu kugeuza mwelekeo kwa kufanya watu wasahau kuhusu uhusiano wa Rais wa Marekani Donald Trump na Epstein.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



