Sudan Kusini yahifadhi wakimbizi na watafuta hifadhi zaidi ya 613,000

(CRI Online) Februari 27, 2026

Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) limesema jana Alhamisi kwamba hadi kufikia mwezi Januari Sudan Kusini inahifadhi wakimbizi na watafuta hifadhi 613,710 katika kaya 164,574 za maeneo 29 kote nchini, likiongeza kuwa jumla ya idadi hiyo inajumuisha wakimbizi 610,268 waliosajiliwa na wanaotafuta hifadhi 3,442.

“Wengi wao, asilimia 94 au watu 576,672, ni wakimbizi wa Sudan, ikifuatiwa na 14,677 au asilimia 2 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, 6,599 kutoka Ethiopia, 5,605 kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati, 5,165 kutoka Eritrea, na 1,550 kutoka mataifa mengine.” UNHCR imesema katika ripoti yake ya hivi iliyotolewa Juba, nchini Sudan Kusini.

Imesema serikali ya Sudan Kusini inaendelea kutoa kipaumbe katika kuwapa hadhi ya ukimbizi wale wanaokimbia kutoka Sudan ili kukabiliana na mgogoro unaoendelea.

Kwa mujibu wa UNHCR, asilimia 49 ya wakimbizi hao ni wanawake wenye umri wa kati ya miaka 0-59, huku wanawake na watoto wakijumlishwa pamoja wanachukua asilimia 75 ya jumla yote.

Shirika hilo limesema Waethiopia na Waeritrea kila upande unachukua asilimia 37 ya jumla, wakitengeneza makundi mawili makubwa zaidi ya waomba hifadhi, wakifuatiwa na Warundi wenye asilimia 9, Waganda wenye asilimia 7, na asilimia 9 ya mataifa mengine.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha