Lugha Nyingine
Afrika Magharibi yalenga usalama wa chakula na utoaji wa ajira katika mashauriano ya ECOWAS nchini Sierra Leone
Viongozi wa Afrika Magharibi na washirika wa maendeleo wameahidi kubadilisha kilimo kuwa chachu ya usalama wa chakula na utoaji wa ajira katika mashauriano ya ngazi ya juu ya Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) yaliyofanyika Alhamis huko Freetown nchini Sierra Leone.
Mkutano huo, wenye kaulimbiu "Kusukuma mbele Mafungamano ya Kiuchumi wa Kikanda Kupitia Mageuzi ya Kilimo, Biashara ya Kikanda na Maendeleo ya Sekta Binafsi", uliwaleta pamoja watunga sera, watendaji wa sekta binafsi na wataalamu wa kilimo kutoka kote katika kanda hiyo.
Akihutubia kwenye mkutano huo, Mwakilishi Mkazi wa ECOWAS nchini Sierra Leone John Azumah amesisitiza kuwa kilimo lazima kiwe kiini cha azma ya muda mrefu ya jumuiya hiyo ya kuanzisha soko la pamoja linalofanya kazi kikamilifu, akiongeza kuwa mkutano huo utasaidia kuoanisha mipango ya maendeleo ya kitaifa na ajenda pana ya mafungamano ya ECOWAS.
Mkutano huo unatarajiwa kutoa mapendekezo yanayoweza kutekelezwa ili kubadilisha kilimo kuwa sekta ya kisasa, yenye ushindani na jumuishi, na kuimarisha maono ya ECOWAS ya kuwa soko la pamoja linaloendeshwa na ukuaji endelevu na ustawi wa pamoja.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



