Mapigano kati ya Pakistan na Afghanistan yaendelea na watu waliouawa na kujeruhiwa waongezeka

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 28, 2026

ISLAMABAD/KABUL - Jeshi la Pakistan limesema kwamba watu 274 wenye silaha wa Afghanistan wameuawa na zaidi ya 400 wamejeruhiwa katika mapigano ya mpakani tokea Alhamisi.

Luteni Jenerali Ahmed Sharif Chaudhry, mkurugenzi mkuu wa Idara ya Uhusiano kwa Umma (ISPR), idara ya vyombo vya habari ya Jeshi la Pakistan, amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari jana Ijumaa kwamba watu wenye silaha wa Afghanistan walifyatua risasi na kuanzisha mashambulizi halisi dhidi ya sehemu 53 katika maeneo 15 kwenye mpaka wa Pakistan na Afghanistan.

Amesema vikosi vya usalama vya Pakistan "vilirudisha nyuma kwa ufanisi" mashambulizi hayo na kuanzisha mashambulizi makini ya kulipiza.

Msemaji huyo amesema kuwa jeshi la anga la Pakistan lilifanya mashambulizi kutoka angani dhidi ya maeneo 22 ya Afghanistan, yakiwemo pamoja na majimbo ya Kabul, Kandahar, Paktia, Nangarhar, Khost na Paktika.

Amesema mashambulizi hayo yalipiga makao makuu ya kijeshi, vituo vya brigade na batalioni, maghala ya silaha, vituo vya ugavi na maficho vinavyodaiwa kutumiwa na watu wenye silaha. Amesema askari 12 wa Pakistani wameuawa, 27 wamejeruhiwa na mmoja bado haijulikani alipo.

Chaudhry amezishutumu utawala wa Taliban wa Afghanistan kwa kuunga mkono watu wenye silaha walioanzisha mashambulizi ndani ya Pakistan, wakiwemo pamoja na watu wa kundi la Tehreek-e-Taliban Pakistan (TTP) lililopigwa marufuku.

Zabihullah Mujahid, msemaji wa serikali ya Afghanistan, alisema Ijumaa kwenye mkutano na waandishi wa habari kuhusu hali wasiwasi ya mpakani kwamba wakati wa operesheni za kulipiza kisasi, askari 55 wa Pakistani wameuawa na wengine kadhaa wamekamatwa.

Mujahid ameeleza kuwa ndege za upelelezi za Pakistan bado zinaruka ndani ya anga ya Afghanistan, na kama Pakistan itaendelea na uchokozi wake, vikosi vya Imarati ya Kiislamu vina uwezo wa kukabiliana kwa hatua kali.

Mujahid amesema, serikali ya Afghanistan imekuwa ikisisitiza mara kwa mara suluhu ya amani na inaendelea kutetea mbinu ya kiujenzi, isiyo ya mabavu katika kutatua hali hiyo.

Katika miaka ya hivi karibuni, hali wasiwasi inazidi kuwa mbaya kati ya nchi hizo mbili, wakati mapigano ya kimabavu yakipamba moto katika sehemu za mpakani za nchi hizo mbili.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha