China yataka kusitishwa mara moja kwa operesheni za kijeshi dhidi ya Iran

(CRI Online) Machi 02, 2026

Wizara ya Mambo ya Nje ya China imesema kushambulia na kumuua Kiongozi Mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei, kumekiuka vibaya mamlaka na usalama wa Iran, na kupuuza Katiba ya Umoja wa Mataifa na kanuni za kimsingi za uhusiano wa kimataifa, na China inapinga na kulaani vitendo hivyo.

Wizara hiyo pia imesisitiza kuwa operesheni za kijeshi dhidi ya Iran zinapaswa kusimamishwa mara moja ili kuepuka hali ya wasiwasi kuongezeka zaidi na kulinda kwa pamoja amani na utulivu wa Mashariki ya Kati na dunia.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha