Kazi ya kutandaza reli kwenye sehemu ya Yunnan ya reli ya mwendo-kasi ya Chongqing-Kunming, China yaanza (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 19, 2026
Kazi ya kutandaza reli kwenye sehemu ya Yunnan ya reli ya mwendo-kasi ya Chongqing-Kunming, China yaanza
Wafanyakazi wakionekana kwenye kazi ya kutandaza reli kwenye sehemu ya ujenzi wa reli ya mwendo-kasi ya Chongqing-Kunming katika Wilaya ya Songming ya Kunming, Mkoa wa Yunnan, kusini magharibi mwa China, Machi 18, 2026. (Xinhua/Hu Chao)

Jozi ya kwanza ya reli za chuma zenye urefu wa mita 500 zimetandazwa tayari bila hitilafu kwenye njia ya reli jana Jumatano, ikionesha kuanza rasmi kwa kazi ya kutandaza reli kwenye sehemu ya Yunnan ya reli ya mwendo-kasi ya Chongqing-Kunming nchini China.

Baada ya kukamilika kwa ujenzi wa reli hiyo ya mwendo-kasi, muda wa kusafiri kati ya Chongqing na Kunming utapunguzwa kwa kiasi kikubwa.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha