Lugha Nyingine
Mji wa Shenzhen, China wazindua mradi wa "Park BOX" ili kuboresha mazingira ya bustani ya wananchi (7)
(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 03, 2026
![]() |
| Watalii wakifurahia chakula na vinywaji kwenye duka chini ya mradi wa "Park BOX" katika Bustani ya Ghuba ya Shenzhen, Shenzhen, Mkoa wa Guangdong, kusini mwa China, Machi 29, 2026. (Xinhua/Mao Siqian) |
Katika miaka ya hivi karibuni, Mji wa Shenzhen, katika Mkoa wa Guangdong, kusini mwa China umeboresha mazingira ya bustani za wananchi kwa kuongeza mambo mbalimbali ya kufanywa na wanachi kwenye bustani za jadi.
Ikiwa ni sehemu ya juhudi hizo, mji huo umezindua mradi wa "Park BOX" kwenye Bustani ya Ghuba ya Shenzhen, ambao una maeneo mbalimbali ya umma pamoja na usanifu wa kisanaa na miundombinu za kutoa urahisi kama vile baa za vitabu na huduma za kuwasilisha oda kwa kutumia droni.
Mji huo pia umetumia kikamilifu rasilimali kutoka maeneo ya kibiashara ya karibu ili kuzijumuisha vema nafasi za kiikolojia katika maisha ya mjini, kukidhi mahitaji ya umma ya kufurahia mazingira mbalimbali na yenye ubora wa hali ya juu ya bustani.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




