Lugha Nyingine
China na Tanzania zatoa heshima kwa raia wa China waliofariki katika ujenzi wa reli ya TAZARA (3)
DAR ES SALAAM - China na Tanzania zimewakumbuka kwa pamoja wataalamu wa China waliojitolea maisha yao wakati wa ujenzi wa Reli ya Tanzania-Zambia (TAZARA), zikiadhimisha miaka 50 ya uendeshaji wa kibiashara wa reli hiyo.
Watu mashuhuri kutoka nchi hizo mbili walikusanyika Jumamosi katika eneo la Makaburi ya Wataalamu wa China jijini Dar es Salaam, ambapo waliweka mashada ya maua kwenye makaburi ya mashujaa hao waliofariki kwa kueleza hisia zao za kuwakumbuka na kutoa heshima kwao wakati wa Siku ya Qingming, ambayo ni siku ya jadi ya China ya kufagia makaburi na kutoa heshima kwa marehemu na kuwakumbuka mababu.
Akizungumza kwenye shughuli hiyo, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Tanzania Patrobas Katambi ameisifu reli hiyo ya TAZARA kuwa ni "ushuhuda hai wa ushirikiano wa Kusini-Kusini" na ni alama ya urafiki wa kudumu kati ya Tanzania na China.
Amesisitiza ni lazima kulinda na kuifanya reli hiyo kuwa ya kisasa na kuiweka kuwa sehemu ya mpango wa ustawishaji.
Balozi wa China nchini Tanzania Chen Mingjian amesema kuwa wafanyakazi zaidi ya 50,000 wa China walishiriki katika ujenzi wa reli hiyo katika miaka ya 1970, ambapo 70 kati yao walijitolea mihanga katika wakati wa ujenzi wa reli.
"Wahanga hawa ni mashujaa waliojenga mnara wa urafiki wa kati ya China na Tanzania na China na Afrika," amesema.
Pia katika shughuli hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania-Zambia Bruno Ching'andu na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania James Kinyasi Millya walitoa shukrani kwa China, wakisifu urafiki wa jadi kati ya nchi hizo mbili.

Ndege wa Kwarara waingia msimu wa kuzaliana huko Shaanxi, China

Eneo la kaboni-sifuri katika Mkoa wa Hainan laonyesha vitendo vya kijani vya China

Vifaa vya kisasa vya usafi vyatoa huduma kwenye Mkutano wa Mwaka wa Jukwaa la Boao la Asia 2026

Eneo Jipya la Xiong'an la China labadilika kuwa mji wenye nguvu hai kutoka mpango
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
