Lugha Nyingine
Kupanda kwa bei za mafuta kwawabana Watanzania huku athari ya migogoro ya Mashariki ya Kati ikiendelea (5)
![]() |
| Watu wakisafiri kwa basi dogo jijini Dar es Salaam, Tanzania, Aprili 4, 2026. (Picha na Emmanuel Herman/Xinhua) |
DAR ES SALAAM - Kila asubuhi kabla ya jua kuchomoza, Herry Msese huendesha basi lake dogo la abiria kupitia mitaa ya Dar es Salaam, Tanzania, akisafirisha abiria kadhaa kwenye njia yenye pilika nyingi.
Hata hivyo, katika wiki za hivi karibuni, mafuta yameibuka kuwa wasiwasi wake mkubwa.
"Hii ni changamoto kubwa," amesema dereva huyo wa dala dala. "Kila siku, lazima niwasilishe shilingi 110,000 za Kitanzania (dola za Marekani karibu 43) kwa mmiliki wa gari."
Awali, gharama za mafuta zilikuwa wastani wa shilingi takriban 90,000 kwa siku, lakini hivi karibuni zimefikia shilingi takriban 150,000.
Katika siku nzuri, kipato ambacho basi linaweza kupata ni shilingi 260,000 tu. "Hii ina maana kwamba karibu kila kitu ninachopata kinatumika kwenye mafuta," amesema.
Ongezeko hilo kubwa la ghafla la bei ya mafuta linafuatia kuzidi kupamba moto kwa mivutano ya siasa za kijiografia katika Mashariki ya Kati inayohusisha Marekani, Israel, na Iran. Minyororo ya usambazaji wa mafuta duniani iliyovurugika imesababisha bei ya mafuta ghafi kupanda na kuathiri nchi zinazoagiza mafuta kama Tanzania.
"Sijui nini kifanyike," Msese ameongeza. "Labda serikali inapaswa kupunguza kodi, au bei ya mafuta inapaswa kushuka. Muhimu zaidi, vita hivi vinapaswa kuisha."
Baada ya kugharamia gharama zote za siku, alikuwa amebaki na shilingi 7,000 pekee. "Kama mambo yatakuwa mabaya zaidi, huenda nikalazimika kutafuta kazi nyingine."
Tanzania inapitia moja ya maongezeko makubwa zaidi ya bei ya mafuta katika miaka ya hivi karibuni, kutokana na mapitio ya hivi karibuni ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji ya Tanzania.
Chini ya muundo mpya wa bei, petroli sasa inauzwa kwa shilingi 3,820 kwa lita, kutoka shilingi 2,864 mwezi Machi. Dizeli imepanda hadi shilingi 3,806, huku mafuta ya taa sasa yakigharimu shilingi 3,684 kwa lita.
Ongezeko hilo kubwa la bei ya mafuta linaenea kwa kasi katika uchumi wa Tanzania, na kuathiri usafirishaji, gharama za chakula, na bajeti za kaya.
Mathalani, katika Soko la Kariakoo, kitovu kikuu cha biashara jijini Dar es Salaam, Erick Matemba alikuwa akijitahidi kudumisha biashara yake ya simu za mkononi.
"Simu nyingi tunazouza zinaagizwa kutoka Dubai. Lakini kwa wiki takriban tatu sasa, hatujapokea mzigo mpya," amesema Mtanzania huyo mwenye umri wa miaka 35.
Mivurugiko hiyo ya usambazaji imepunguza usafirishaji kwa meli, na kusababisha uhaba wa simu na vifaa. Gharama kubwa zaidi za mafuta pia zimeongeza gharama za kuwasilisha bidhaa kwa wateja, huku safari ambayo hapo awali iligharimu shilingi 5,000 sasa ikifikia shilingi takriban 8,000.
"Tunalazimika kuongeza bei kidogo ili kufidia gharama hizi," Matemba ameelezea.
Wachumi wanaonya kwamba kupanda huko kwa bei za mafuta kunaweza kusababisha shinikizo kubwa la mfumuko wa bei. Kadri gharama za usafiri na uzalishaji zinavyozidi kuongezeka, biashara zinaweza kuwapa watumiaji gharama hizo.

Ndege wa Kwarara waingia msimu wa kuzaliana huko Shaanxi, China

Eneo la kaboni-sifuri katika Mkoa wa Hainan laonyesha vitendo vya kijani vya China

Vifaa vya kisasa vya usafi vyatoa huduma kwenye Mkutano wa Mwaka wa Jukwaa la Boao la Asia 2026

Eneo Jipya la Xiong'an la China labadilika kuwa mji wenye nguvu hai kutoka mpango
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
