Chai nyeupe yaingia msimu wa mavuno katika Wilaya ya Anji, Zhejiang, China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 09, 2026
Chai nyeupe yaingia msimu wa mavuno katika Wilaya ya Anji, Zhejiang, China
Picha hii iliyopigwa Aprili 8, 2026 ikionyesha wafanyakazi wakichuma majani ya chai kwenye shamba la chai katika Wilaya ya Anji, Mkoa wa Zhejiang, mashariki mwa China. (Xinhua/Huang Zongzhi)

Hivi sasa chai nyeupe katika Wilaya ya Anji, Mkoa wa Zhejiang, mashariki mwa China imeingia msimu wake wa mavuno. Mwaka 2025, uzalishaji wa chai nyeupe katika wilaya hiyo ya Anji ulifikia tani 2,630, huku thamani ya mapato ya mwaka ya mnyororo wa shughuli za chai ikizidi yuan bilioni 7 (dola za Marekani karibu bilioni 1.02). Wilaya hiyo pia iliwapokea watalii wanaotembelea shamba la chai kwa zaidi ya mara milioni 5 mwaka jana.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha