Wajasiriamali vijana wachangia ustawi wa vijiji huko Jiaxing mkoani Zhejiang, China (6)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 09, 2026
Wajasiriamali vijana wachangia ustawi wa vijiji huko Jiaxing mkoani Zhejiang, China
Watu wakiwa wamepumzika kwenye eneo maalum la kutengeneza na kuuza mikate katika mji mdogo wa Yuxin ulioko Eneo la Nanhu la Mji wa Jiaxing, Mkoa wa Zhejiang, mashariki mwa China. (Xinhua/Xu Yu)

Katika miaka ya hivi karibuni, Eneo la Nanhu la Mji wa Jiaxing, Mkoa wa Zhejiang, mashariki mwa China limekuwa likitoa uungaji mkono wa kisera, msaada wa kujenga majukwaa, na uleaji na ukuzaji wa biashara kwa wajasiriamali vijana wanaorudi maskani yao, pamoja na kuwapa nafasi za kuanzisha shughuli zao kwa gharama chini, hali ambayo imewavutia mamia ya vijana kurudi maskani yao kuanzisha biashara zao.

Wajasiriamali hao vijana ni wenye mawazo ya kutumia mtandao wa intaneti, mantiki ya biashara ya kisasa, na kuelewa mfumo wa biashara ya kivumbuzi, ndiyo wamebadilisha mashamba na nyumba za vijijini kuwa bidhaa za kitamaduni na utalii.

Wameanzisha mambo ya kuvuma mtandaoni kama vile masoko ya sanaa, mkate uliookwa kwenye tanuru, mikahawa ya vijijini, kucheza na wanyama kipenzi, na karakana za utoaji mafunzo vijijini, hayo yote yamesaidia wanakijiji kunadi na kuuza mazao ya kilimo yenye sifa pekee, na kuongeza mapato ya wenyeji.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha