Xinjiang yaweka viota vya Ndege ili kutunza ndege wanaohamahama na kuhifadhi Nyaya za Umeme (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 10, 2026
Xinjiang yaweka viota vya Ndege ili kutunza ndege wanaohamahama na kuhifadhi Nyaya za Umeme
Picha iliyopita Aprili 8, 2026 ikionesha ndege wanaohamahama wakicheza kwa furaha kwenye Bustani ya Kitaifa ya Ardhi Oevu ya Ziwa Ulunggur iliyoko Wilaya ya Fuhai ya eneo la Altay, Mkoa Unaojiendesha wa Kabila la Wauygur wa Xinjiang, China. (Nurbek Nurman/Xinhua)

Eneo la Altay lina mfumo mkubwa wa maji na mazingira mazuri ya asili, likiwa ni makazi muhimu kwa ndege wanaohamahama. Kadiri hali ya hewa inavyozidi kuwa joto, eneo hilo limeingia katika kipindi cha kuhama kwa ndege wengi sana, ambapo shughuli za ndege zinazoongezeka zimeleta changamoto zaidi kwa uendeshaji salama wa nyaya za kusambaza umeme za eneo hilo.

Ili kukabiliana na changamoto hizi, Kampuni ya Gridi ya China tawi la Altay imeanzisha operesheni maalum. Wafanyakazi wametumia droni kufunga viota 16 vya ndege vya kiikolojia kando ya njia muhimu za kusambaza umeme, ili kuzuia ndege kujenga viota kwenye miundombinu ya umeme, na hivyo kuepusha hatari zinazoweza kujitokeza.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha