Lugha Nyingine
Siku ya Lugha ya Kichina ya UN yaadhimishwa nchini Kenya kwa wito wa mazungumzo ya kistaarabu (3)
![]() |
| Wasanii wakifanya onyesho kwenye shughuli ya kuadhimisha Siku ya Lugha ya Kichina ya Umoja wa Mataifa katika Ofisi ya Umoja wa Mataifa, Nairobi (UNON) nchini Kenya, Aprili 13, 2026. (Xinhua/Liu Qiong) |
NAIROBI – Siku ya 17 ya Lugha ya Kichina ya Umoja wa Mataifa kwa mwaka huu wa 2026 imesherehekewa jana Jumatatu jijini Nairobi, Kenya, kwa wito wa kuhimiza mazungumzo kati ya tamaduni na ustaarabu mbalimbali.
Shughuli hiyo ilifanyika katika Ofisi ya Umoja wa Mataifa jijini Nairobi (UNON) chini ya kaulimbiu ya "Lugha ya Kichina Hudumu, Ustaarabu Hung'aa," ambapo wanadiplomasia, wasomi, na wanafunzi walikusanyika pamoja na kuhimiza mazungumzo na maelewano duniani.
Balozi wa China nchini Kenya Guo Haiyan amesema maandiko ya lugha ya Kichina yana historia ndefu na ni mojawapo ya aina za sanaa wakilishi zaidi za lugha ya Kichina.
Maandiko ya lugha ya Kichina yanaonesha maadili ya "mapatano katika uanuwai," yanaonyesha mtazamo wa ustaarabu kuhusu "usawa na kufundishana," na yanawasilisha mtazamo wa dunia wa kuishi pamoja katika hali ya mapatano.
Akisema, mwaka 2026 ni Mwaka wa maelewano kati ya Watu wa China na wa Afrika na kufundishana kati ya ustaarabu mbalimbali ni muhimu kwa ajili ya kusukuma mbele ujenzi wa mambo ya kisasa, na amesema lugha ya Kichina inakuwa "ufunguo wa dhahabu" ambao unafungua fursa barani Afrika na Kenya.
Mkurugenzi Mkuu wa UNON Zainab Hawa Bangura amesema kwamba Siku ya Lugha ya Kichina inayoadhimishwa katika mfumo wa Umoja wa Mataifa, inasisitiza maoni ya pamoja yanayozidi kuongezeka juu ya hitaji la kutumia nguvu za lugha nyingi kwa kuimarisha utaratibu wa dunia unaofuata kanuni.
"Ikiwa ni moja ya lugha sita rasmi za Umoja wa Mataifa, lugha ya Kichina inahusu mali nyingi za urithi wa kitamaduni na kiakili na kuonesha maadili ya mapatano, kuheshimiana na kuwajibika pamoja, kanuni hizi ambazo zinaendana kwa kina na dhamira ya shirika hili," Bangura amesema.
"Kwa hiyo, maadhimisho ya leo yanasisitiza umuhimu wa mawasiliano ya kitamaduni katika kuzidisha uhusiano kati ya Afrika, China, na jumuiya pana ya kimataifa, na katika kusukuma mbele moyo wa washirika ambao unaunga mkono kazi yetu," ameongeza.
Shughuli hiyo pia imehusisha maonyesho mbalimbali ya kiutamaduni, yakiwemo maonesho ya kusoma mashairi, kufanya michezo ya Wushu, kupiga ngoma, na kuandika maandiko ya lugha ya Kichina.

Ndege wa Kwarara waingia msimu wa kuzaliana huko Shaanxi, China

Eneo la kaboni-sifuri katika Mkoa wa Hainan laonyesha vitendo vya kijani vya China

Vifaa vya kisasa vya usafi vyatoa huduma kwenye Mkutano wa Mwaka wa Jukwaa la Boao la Asia 2026

Eneo Jipya la Xiong'an la China labadilika kuwa mji wenye nguvu hai kutoka mpango
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
