Lugha Nyingine
"Kufunzana kati ya Ustaarabu" - Maonyesho ya Vinyago vya Afrika Yafanyika Beijing, China (8)
Aprili 12, maonyesho ya "Kufunzana kati ya Ustaarabu" — Maonyesho ya Sanaa za Vinyago vya Afrika kutoka kwenye ukusanyaji wa Jumba la Makumbusho ya Sanaa ya Kitaifa ya China" yalifunguliwa kwenye Jumba la Makumbusho ya Sanaa ya Kitaifa ya China mjini Beijing.
Yakiwa ni mradi muhimu wa "Mwaka wa Mawasiliano ya Kitamaduni kati ya Watu wa China na Afrika 2026," maonyesho hayo yanaandaliwa kwa ushirikiano na Jumuiya ya China kwa ajili ya Mabadilishano ya Kitamaduni na Nchi za Nje na Jumba la Makumbusho ya Sanaa ya Kitaifa ya China. Yanaonyesha kazi maridadi jumla ya 128—zikiwemo vinyago, sanaa za kuchongwa kwa shaba, na uchoraji—iliyosanifiwa na wasanii kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika (yakiwemo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Tanzania, Msumbiji, Côte d'Ivoire, Benin, Ghana, Kenya, na Nigeria) vilevile wasanii wa China walioteuliwa.
Maonyesho hayo yanawasilisha kwa kina mvuto wa kipekee wa sanaa za kuchongwa za Afrika na umuhimu mkubwa katika mazungumzo kati ya ustaarabu wa China na Afrika. Maonyesho hayo yamepangwa kuendelea hadi Aprili 22.

Ndege wa Kwarara waingia msimu wa kuzaliana huko Shaanxi, China

Eneo la kaboni-sifuri katika Mkoa wa Hainan laonyesha vitendo vya kijani vya China

Vifaa vya kisasa vya usafi vyatoa huduma kwenye Mkutano wa Mwaka wa Jukwaa la Boao la Asia 2026

Eneo Jipya la Xiong'an la China labadilika kuwa mji wenye nguvu hai kutoka mpango
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
