Lugha Nyingine
Wasichana wanafunzi Watanzania wafuatilia ndoto kupitia kujifunza lugha ya Kichina (3)
![]() |
| Mwanafunzi akiandika ubaoni kwenye darasa la lugha ya Kichina katika Shule ya Sekondari ya Zanaki jijini Dar es Salaam, Tanzania, Aprili 15, 2026. (Xinhua/Emmanuel Herman) |
DAR ES SALAAM – Ndani ya darasa kwenye Shule ya Sekondari ya Zanaki, shule ya wasichana inayomilikiwa na serikali jijini Dar es Salaam, Tanzania, Rosemary Thadei Mushi mwenye umri wa miaka 13 anasimama miongoni mwa wenzake, akiwaongoza kwa umakini kupitia toni za lugha sanifu ya Kichina.
Kote shuleni hapo, wanafunzi wanazidi kukumbatia lugha ya Kichina si tu kama somo la kitaaluma, bali kama njia ya kuelekea fursa za siku za baadaye. Dunia inapojiandaa kuadhimisha Siku ya Lugha ya Kichina, shauku hiyo miongoni mwa wanafunzi hao inaonyesha mwelekeo mpana kote Afrika, ambako uhitaji katika kujifunza lugha hiyo unaendelea kuongezeka.
Kwa Rosemary, mwanafunzi wa Kidato cha Kwanza, kusoma Kichina tayari kumeanza kubadilisha mtazamo wake. Zaidi ya kuwa mjuzi wa herufi na matamshi, amejenga uelewa mpana zaidi wa utamaduni na watu wa China.
Akiwa na matamanio ya kuwa daktari, anaamini ujuzi katika lugha hiyo unaweza kumsaidia kupata ufadhili wa masomo ya kusoma nje ya nchi na kupanua upeo wake.
Koletha Fikiri Mtakuja mwenye umri wa miaka 15 ana maono kama hayo. Akiwa mwanafunzi wa kidato cha tatu mwenye matarajio makubwa katika uhandisi, anaiona lugha ya Kichina kama lango la kufikia maendeleo ya kiteknolojia ya China.
"China imepiga hatua sana katika sayansi na teknolojia," Koletha amesema. "Kujua Kichina kutanisaidia kujifunza moja kwa moja kutoka kwa wahandisi wao."
Wanafunzi wote hao wawili wanaota kutembelea China, wakitarajia kutembea kwenye Ukuta Mkuu mjini Beijing na kujionea ana kwa ana mila na maendeleo ya haraka wanayokumbana nayo kwa sasa kupitia majukwaa ya kidijitali, muziki, na filamu.
Matarajio yao hayo makubwa yanaendana na vuguvugu pana duniani. Siku ya Lugha ya Kichina, ambayo huadhimishwa kila mwaka Aprili 20, ilianzishwa na Umoja wa Mataifa ili kuhimiza lugha mbalimbali na matumizi sawa ya lugha zake sita rasmi. Katika miaka ya hivi karibuni, siku hiyo pia imekuwa yenye kuashiria uhusiano unaokua wa kielimu na kiuchumi kati ya China na Afrika.
Nyuma ya maendeleo ya wanafunzi hao kuna mwalimu wao, Ema Silagomi, mmoja wa waelimishaji waanzilishi wa lugha ya Kichina wa Tanzania ambaye alisoma katika Chuo Kikuu cha Mambo ya Anga cha Zhengzhou na Chuo Kikuu cha Henan vya China, ambako alipata ujuzi wa lugha hiyo na mbinu za kufundishia.
"Niliona fursa nchini China kuhusu elimu, biashara, na mabadilishano ya kitamaduni, na nilitaka vijana wa Tanzania wanufaike," Silagomi ameelezea. "Ni lugha iliyojaa fursa."

Ndege wa Kwarara waingia msimu wa kuzaliana huko Shaanxi, China

Eneo la kaboni-sifuri katika Mkoa wa Hainan laonyesha vitendo vya kijani vya China

Vifaa vya kisasa vya usafi vyatoa huduma kwenye Mkutano wa Mwaka wa Jukwaa la Boao la Asia 2026

Eneo Jipya la Xiong'an la China labadilika kuwa mji wenye nguvu hai kutoka mpango
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
