Kundi jipya la mabaki ya askari wahanga wa China katika Vita vya Korea kurudishwa leo Jumatano (4)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 22, 2026
Kundi jipya la mabaki ya askari wahanga wa China katika Vita vya Korea kurudishwa leo Jumatano
Picha hii iliyopigwa Aprili 21, 2026 ikionyesha maneno ya kukaribisha kurudishwa kwa mabaki ya askari wa Jeshi la Kujitolea la Watu wa China (CPV) kutoka Korea Kusini mjini Shenyang, Mkoa wa Liaoning, kaskazini mashariki mwa China. (Xinhua/Li Gang)

BEIJING – Wizara ya Mambo ya Wanajeshi waliostaafu ya China imesema, Mabaki ya askari wahanga 12 wa Jeshi la Kujitolea la Watu wa China (CPV) waliouawa katika Vita vya Kupinga Uchokozi wa Marekani na Kuisaidia Korea (1950-1953) yatarudishwa China kutoka Korea Kusini leo Jumatano.

Ndege kubwa ya usafirishaji ya Y-20B ya Kikosi cha Anga cha Jeshi la Ukombozi wa Umma la China itawabeba mashujaa hao waliofariki hadi Shenyang, mji mkuu wa Mkoa wa Liaoning, kaskazini mashariki mwa China, ambapo ni maskani ya makaburi ya mashujaa wa CPV.

Hii ni mara ya kwanza kwa ndege hiyo ya Y-20B kubeba jukumu hilo la kurudisha mabaki ya mashujaa hao nyumbani. Baada ya kuingia tena katika anga ya China, ndege hiyo itasindikizwa na ndege nne za kivita za J-20.

Hii itakuwa mara ya 13 kurudishwa kwa mabaki ya CPV kufuatia makubaliano ya makabidhiano kati ya nchi hizo mbili. Tangu 2014, mabaki ya askari 1,011 yamesharudishwa nchini China kutoka Korea Kusini, wizara hiyo imesema.

China imeongeza juhudi za kutambua mabaki ya wahanga hao wa CPV, ikiwa ni pamoja na kuundwa kwa kanzidata ya DNA kwa ajili ya wahanga hao na jamaa zao, na kutoa uungaji mkono thabiti wa kiufundi na data ili kusaidia familia zaidi kuwapata wapendwa wao wasiojulikana waliko.

China ilituma wanajeshi milioni 2.9 wa CPV kuisaidia Jamhuri ya Watu ya Kidemokrasia ya Korea wakati wa vita, ambapo miongoni mwao zaidi ya 360,000 waliuawa au kujeruhiwa katika vita.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha