Lugha Nyingine
Mkutano wa Kwanza wa Wajasiriamali wa China na Afrika wafanyika katika makao makuu ya AU ukitoa wito wa kujiendeleza kwa pamoja
ADDIS ABABA – Mkutano wa Kwanza wa Wajasiriamali wa China na Afrika umefanyika jana Jumanne katika makao makuu ya Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia, kwa kutoa wito wa kuimarisha ushirikiano kati ya China na Afrika ili kuhakikisha maendeleo kwa pamoja.
Mkutano huo ulioandaliwa kwa pamoja na Ujumbe wa China ulioko katika AU, Kamati ya AU na Shirikisho la Wafanyabiashara wa China barani Afrika, na pia kwa ushirikiano na washirika wengine, mkutano huo umefanyika chini ya kaulimbiu ya "Kuzidisha Ushirikiano wa Kufuata Hali Halisi kati ya China na Afrika na Kuanza Safari Mpya kwa Maendeleo," ambapo viongozi wa AU, maofisa waandamizi wa China na Afrika, wajumbe wa wanadiplomasia wa China na Afrika, pamoja na wajumbe wa wafanyabiashara kutoka pande zote mbili wamehudhuria mkutano huo.
Akihutubia mkutano huo , Mwenyekiti wa Kamati ya AU, Mahmoud Ali Youssouf, amesema bara la Afrika linatambuliwa sana kuwa injini ya ongezeko la uchumi wa Dunia katika siku za baadaye, ikiwa na maliasili nyingi, uwezo mkubwa ambao haujatumika na idadi kubwa ya vijana ya kipekee.
Akipongeza sera ya China ya ushuru-sifuri kwa bidhaa kutoka nchi 53 za Afrika, ametoa wito kwa kampuni za China kuongeza uwekezaji barani Afrika, kufanya ushirikiano chini ya moyo wa kunufaishana na kampuni za Arika ili kujenga minyororo ya thamani na minyororo ya utoaji bidhaa.
Rais wa Ethiopia Taye Atske Selassie amesema kwenye mkutano huo kwamba kutokana na kuanzishwa na kufanya utendaji kwa Eneo la Biashara Huria la Bara la Afrika, Afrika si ahadi ya baadaye tena bali ni uhalisia wa ustawi wa biashara.
Rais huyo amesema, "Twafanye mkutano huu uwe jukwaa ambalo tunawawezesha wajasiriamali wa kizazi kipya wajitokeze, ambapo Afrika na China zitashirikiana bega kwa bega kuelekea mustakabali wa uvumbuzi na ustawi kwa pamoja".
Kwa upande wake, Jiang Feng, mkuu wa Ujumbe wa China ulioko katika AU, amesema, kwa kuwa mwaka huu ni mwanzo wa Mpango wa 15 wa Miaka Mitano wa China, unaleta matarajio makubwa kwa ajili ya ushirikiano wa kina kati ya China na Afrika katika sekta ya biashara.
Amesema China itatekeleza hatua za ushuru-sifuri kwenye utozaji wa ushuru kwa bidhaa zote kutoka nchi zote 53 za Afrika zenye uhusiano wa kidiplomasia nayo kuanzia Mei 1, jambo ambalo litasaidia kutandika njia ya kulibadilisha soko kubwa la China kuwa fursa kubwa kwa bidhaa za Afrika zenye ubora wa hali ya juu.
Washiriki kwenye mkutano huo wametoa wito kwa wajasiriamali kutoka sekta zote katika pande zote mbili kushiriki kwa juhudi katika mawasiliano na ushirikiano, kutumia vya kutosha hatua za ushuru-sifuri, makubaliano ya uwekezaji kirahisi, na majukwaa mbalimbali ya mazungumzo ya uchumi na biashara, na kutafuta fursa mpya kwa ajili ya ushirikiano.

Ndege wa Kwarara waingia msimu wa kuzaliana huko Shaanxi, China

Eneo la kaboni-sifuri katika Mkoa wa Hainan laonyesha vitendo vya kijani vya China

Vifaa vya kisasa vya usafi vyatoa huduma kwenye Mkutano wa Mwaka wa Jukwaa la Boao la Asia 2026

Eneo Jipya la Xiong'an la China labadilika kuwa mji wenye nguvu hai kutoka mpango
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
