Lugha Nyingine
Taka za nyumbani zabadilishwa kuwa umeme wa kijani katika Mkoa wa Hunan, China (3)
Bustani ya ulinzi wa mazingira ya Heimifeng ni eneo maalum kubwa la viwanda jumuishi la ulinzi wa mazingira lililoko katika eneo la Wangcheng la Mji wa Changsha, Mkoa wa Hunan, katikati mwa China.
Uwezo wa eneo hilo wa kuchakata taka za nyumbani unafikia tani 10,000 kila siku, na ule wa uchafu wa majimaji ni tani 1,000 kwa siku. Kupitia uchomaji taka, eneo hilo maalum linazalisha umeme wa kijani kwa kilowati-saa zaidi ya bilioni 1.7 kwa mwaka na kupunguza uzalishaji wa kaboni dioksidi kwa tani zaidi ya milioni 1.2 kila mwaka.
Aidha, eneo hilo maalumu likiwa kituo cha uenezi wa elimu ya sayansi ya mazingira katika mkoa huo, tangu mwaka 2021, limepokea watembeleaji zaidi ya 40,000 katika siku za kufunguliwa kwa umma, na kueneza ujuzi kwa umma kuhusu upangaji wa taka tofauti na matumizi ya taka ngumu.

Ndege wa Kwarara waingia msimu wa kuzaliana huko Shaanxi, China

Eneo la kaboni-sifuri katika Mkoa wa Hainan laonyesha vitendo vya kijani vya China

Vifaa vya kisasa vya usafi vyatoa huduma kwenye Mkutano wa Mwaka wa Jukwaa la Boao la Asia 2026

Eneo Jipya la Xiong'an la China labadilika kuwa mji wenye nguvu hai kutoka mpango
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
