Jeshi la Majini la China Lasherehekea Maadhimisho ya Miaka 77 tangu Kuanzishwa Kwake

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 24, 2026
Jeshi la Majini la China Lasherehekea Maadhimisho ya Miaka 77 tangu Kuanzishwa Kwake
Tarehe 21, Aprili, 2026, watu wakishiriki kwenye shughuli ya Siku ya Kufunguliwa kwa umma ya Jeshi la Majini la China huko Dongying, Mkoa wa Shandong wa China. (Xinhua/Wang Guangjie)

Siku ya Alhamisi, China ilisherehekea maadhimisho ya miaka 77 tangu kuanzishwa kwa Jeshi lake la Majini (PLAN). Jeshi hilo linalozidi kuimarishwa kihalisi siku hadi siku imekuwa nguvu muhimu kwa utulivu wa kikanda na Dunia.

Upande wa Jeshi la Majini la China umesema kuwa, Jeshi la Ukombozi la Umma la China (PLA) lilifungua vituo vyake katika miji zaidi ya 10 kwa umma kama sehemu ya shughuli ya maadhimisho hayo, huku likionyesha makumi ya manowari yanayofanya kazi hivi sasa.

Manowari hayo ni pamoja na Manowari ya kurusha makombora (DDG), Manowari sindikizi na Manowari ya uchukuzi ya amphibious, pamoja na manowari za kutoa ugavi, meli za kutoa huduma za matibabu na nyingine za kutoa msaada. Nyingi kati ya manowari hizo zilishiriki katika opereshi za kulinda meli kwenye Ghuba ya Aden, kufanya ziara nje ya nchi, na kushiriki kwenye mazoezi ya kijeshi ya pamoja.

Juhudi za China za kuendeleza jeshi la majini lenye nguvu kubwa zinahusiana moja kwa moja na hali ya kijiografia na historia yake. China ikiwa na mwambao wa bahari wa urefu wa zaidi ya kilomita 18,000 na maeneo mapana ya bahari, ndiyo maana inatilia maanani zaidi kulinda usalama wa maeneo yake ya bahari, na kufanya hivyo kunatokana na mashambulizi zaidi ya mara 470 yaliyofanywa na majeshi ya majini ya nchi mbalimbali katika wakati wa kutoka mwaka 1840 hadi mwaka 1949.

Jeshi la Majini la PLA lilianzishwa mwaka 1949, ambapo Jamhuri ya Watu wa China ilianzishwa mwaka huohuo. Hivi leo, jeshi hilo limeendelezwa kuwa jeshi la mambo ya kisasa la kimkakati lenye aina zote za vikosi vya maji, ambavyo vimekuwa na uwezo wa kupigania vita vya kawaida na uwezo wa kinyuklia.

Katika muda wa zaidi ya miaka kumi tu iliyopita, jeshi la majini la China limejenga manowari tatu za kubeba ndege za kivita. Ya kwanza ni Manowari ya Liaoning, ambayo iliundwa kwa kukarabati manowari iliyoundwa na Soviet Union na kuanza kufanya kazi mwaka 2012; ya pili ni Manowari ya Shandong, iliyoanza kufanya kazi mwaka 2019, ambayo ni manowari ya kwanza ya kubeba ndege za kivita iliyoundwa na China yenyewe.

Manowari ya tatu ya Fujian ya kubeba ndege za kivita, ilianza kazi yake mwezi Novemba 2025 na kwa sasa ndiyo kubwa zaidi kati ya manowari za jeshi hilo zinazofanya kazi. Ujenzi wa kikosi cha jeshi hilo cha ndege zinazobebwa na manowari unaendelea kufanyika, na kikosi hicho kitahusisha ndege za kivita, ndege za kutoa tahadhari mapema, na helikopta zilizoundwa mahususi kwa ajili ya operesheni za manowari ya kubeba ndege.

Mbali na mpango wa manowari ya kubeba ndege, jeshi la majini la China pia limeongeza nyambizi mpya za kimkakati za nyuklia, manowari zenye uwezo mbalimbali za tani 10,000, manowari za kufanya mashambulizi ya amphibious, na manowari za kutoa ugavi ili kusaidia operesheni za baharini na kulinda usalama wa nchi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Deng Jie)

Picha