Lugha Nyingine
Meli ya hospitali ya Jeshi la Majini la China yahudumia watu zaidi ya 26,000 katika jukumu la matibabu nje ya nchi la muda mrefu zaidi (2)
SANYA - Meli ya hospitali ya Silk Road Ark ya Jeshi la Majini la China jana Jumapili ilirudi nyumbani China baada ya kukamilisha jukumu la matibabu la siku 234 nje ya nchi, ambalo ni la muda mrefu zaidi kati ya majukumu kama hilo yaliyotekelezwa na Jeshi la majini la China.
Jukumu la meli hiyo ya hospitali lilipewa jina la "Mission Harmony-2025. " Usafiri wa meli hiyo ulianza Septemba 2025 na ulielekea nchi za Nauru, Fiji, Tonga, Jamaica, Barbados na Papua New Guinea, ambako ilitoa huduma mbalimbali za matibabu bila malipo kwa wakazi wa nchi hizo.
Katika kipindi cha kutekeleza jukumu la meli hiyo, timu ya madaktari wa meli hiyo ya hospitali ilitoa huduma kwa wagonjwa zaidi ya 26,324 na kufanya upasuaji 2,724. Aidha, ilifanya upimaji na uchunguzi wa magonjwa kwa mara 17,273, na kuwapokea wagonjwa 136 kulazwa hospitali.
Wafanyakazi wa meli hiyo ya hospitali walipokuwa katika nchi za Brazil na Chile, pia walifanya shughuli ya kubadilishana mawazo kuhusu matibabu, na walishiriki katika mazoezi ya pamoja kwenye bahari na vikosi vya majini vya majeshi ya Fiji, Tonga na Brazil.
"Mission Harmony" ni mradi wa huduma ya matibabu ya ubinadamu nje ya nchi ulioanzishwa na Jeshi la Majini la China tangu mwaka 2010. Majukumu 10 ya kabla ya hapo yalitekelezwa na meli ya hospitali ya Peace Ark. Jukumu jipya la 11 katika mfululizo huo, linatekelezwa kwa mara ya kwanza na meli hiyo ya hospitali ya Silk Road Ark nje ya nchi.
Ikiwa ni meli ya pili ya hospitali ya kiwango cha kutoa huduma baharini iliyoundwa na China yenye uzito wa tani 10,000, meli ya hospitali ya Silk Road Ark ina vitengo 14 vya matibabu, vitengo saba vya usaidizi na vyumba nane vya kisasa vya kufanyia upasuaji, ambavyo ni vyenye uwezo wa kufanya upasuaji aina zaidi ya 60.
Meli hiyo pia imewekewa helikopta ya uokoaji, inayoweza kufanya operesheni za kukabiliana na hali ya uokoaji wa dharura.
Yote hayo ndani ya meli hiyo ya hospitali yanaunga mkono huduma mbalimbali, ikiwa ni pamoja na upasuaji wa jumla, orthopediki, uzazi na magonjwa ya wanawake, na magonjwa ya macho.
Katika nchi ya Fiji, mwanamume mmoja alitafuta matibabu ndani ya meli hiyo ya hospitali baada ya kupata maumivu ya tumbo yaliyodumu kwa muda mrefu. Timu ya madaktari wa China ilipanga haraka upimaji wa koloni, ambao ulithibitisha saratani ya rektamu.
Madaktari wa China wakishirikiana na madaktari na wataalamu wa ganzi wa nchi hiyo kufanya upasuaji mgumu wa saratani ya rektamu ya kati hadi chini, ambao ulikamilishwa kwa mafanikio.
"Asante, madaktari wa China !" Familia ya mgonjwa huyo ilisema kwa Kichina kutoa shukrani baada ya upasuaji huo.

Ndege wa Kwarara waingia msimu wa kuzaliana huko Shaanxi, China

Eneo la kaboni-sifuri katika Mkoa wa Hainan laonyesha vitendo vya kijani vya China

Vifaa vya kisasa vya usafi vyatoa huduma kwenye Mkutano wa Mwaka wa Jukwaa la Boao la Asia 2026

Eneo Jipya la Xiong'an la China labadilika kuwa mji wenye nguvu hai kutoka mpango
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
