Mkoa wa Hainan, China wajenga maduka 12 yasiyotozwa ushuru chini ya sera ya ununuzi inayoboreshwa (5)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 27, 2026
Mkoa wa Hainan, China wajenga maduka 12 yasiyotozwa ushuru chini ya sera ya ununuzi inayoboreshwa
Wateja wakifanya manunuzi kwenye duka lisilotozwa ushuru huko Haikou mkoani Hainan, kusini mwa China, Aprili 25, 2026. (Xinhua/Pu Xiaoxu)

HAIKOU - Katika miaka 15 iliyopita tangu China ilipoanza kutekeleza sera ya manunuzi yasiyotozwa ushuru kwa bidhaa katika Mkoa wa Hainan, ambao ni mkoa wa kisiwani ulioko kusini kabisa mwa China, mamlaka za forodha zimesimamia thamani ya mauzo ya jumla ya yuan bilioni 286.4 (dola za Marekani karibu bilioni 41.76) ya bidhaa milioni 347 zisizotozwa ushuru ambazo zilinunuliwa na watalii kabla ya kuondoka huko, mamlaka za forodha za mkoa huo zimesema.

Tokea Aprili 20, 2011, sera hiyo imepitia raundi kadhaa za marekebisho na uboreshaji. Hivi sasa, kisiwani Hainan kumekuwa na maduka 12 yasiyotozwa ushuru kwa bidhaa zilizonunuliwa na watalii huko.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha