Lugha Nyingine
Sera ya Ushuru-sifuri ya China yabadilisha maisha ya wakulima wa pilipili wa Rwanda (3)
![]() |
| Mkulima Emmanuel Bihoyiki akichuma pilipili katika Kijiji cha Ibiza Wilaya ya Kayonza, Mkoa wa Mashariki, Rwanda, Aprili 14, 2026. (Xinhua/Ju Yinhe) |
KIGALI - Kwenye mashamba yenye rutuba ya Kijiji cha Ibiza, Wilaya ya Kayonza mashariki mwa Rwanda, safu za pilipili nyekundu zilizostawi ni zaidi ya zao la kuuzwa nje -- zinabadilisha maisha.
Kwa mamia ya wakulima katika wilaya hiyo ya Kayonza, mauzo ya nje ya pilipili yanayozidi kuongezeka ya Rwanda kwenda China yanafungua njia ya kutoka katika umaskini, yakichochewa na sera ya ushuru-sifuri ya China na mahitaji makubwa ya soko la China. Kile kilichoanza kama shughuli ndogo ya kilimo kimekua haraka na kuwa fursa inayobadilisha maisha kwa wakulima, wafanyakazi na wauzaji nje.
Katikati ya mabadiliko haya ni Fisher Global, kampuni ya kilimo ya Rwanda iliyoanza kusafirisha kuuza nje pilipili kavu kwenda China mwaka 2022. Kampuni hiyo imepanuka haraka, ikigeuza pilipili kuwa moja ya mazao ya biashara yenye matumaini zaidi kwa jamii za vijijini.
"Mwanzoni, tulikuwa na hekta takriban 15 tu zinazolimwa pilipili, lakini sasa tumepanuka hadi hekta 300," Herman Uwizeyimana, meneja mkuu wa Fisher Global, ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua kwenye kiwanda cha pilipili cha kampuni hiyo katika Eneo Maalum la Viwanda la Rwamagana, Mkoa wa Mashariki.
Kwa mujibu wa Uwizeyimana, kampuni hiyo sasa ina wafanyakazi wa kudumu 31 na wafanyakazi wa vipindi maalum hadi 600, hali ambayo imetengeneza ajira zinazohitajika sana na kuongeza mapato ya wenyeji.
"Kusafirisha kwenda kuuza China kumekuwa fursa nzuri kwetu. Kwa makubaliano kati ya Rwanda na China ya kusafirisha pilipili kavu, hakika imefungua milango," amesema. "Kuweza kufikia soko kubwa na tulivu la namna hiyo kumetuwezesha kuendelea kuboresha wingi na ukubwa wa eneo letu la kupanda."
Mauzo ya nje ya pilipili ya Fisher Global kwenda China yaliongezeka kutoka kontena moja mwaka 2022 hadi makontena takriban 10 mwaka 2023, na sasa yanafikia tani takriban 300 za pilipili kavu, huku mipango ikizidi tani 1,000 kwa mwaka.
Mabadiliko makubwa yanaonekana miongoni mwa wakulima, kutokana na mapato yao kuongezeka kutokana na kilimo cha pilipili.
Ilikuwa ni kwenye ploti ndogo ambapo Emmanuel Bihoyiki, mkulima mwenye umri wa miaka 28, alianza kulima pilipili mwaka 2021. Leo, analima kwenye ploti ya ukubwa wa zaidi ya hekta mbili.
"Katika mavuno ya kwanza, nilipata faranga milioni moja za Rwanda (karibu dola 685 za Marekani); katika mavuno ya pili, nilipata milioni 2.8; na katika mavuno ya tatu, nilipata milioni 3.5," Bihoyiki amesema.
Utulivu wa soko la China ni sababu muhimu ya mafanikio hayo. Wakulima wanasaini mikataba na Fisher Global kabla ya kupanda mazao ili kuhakikisha kwamba mazao yao yatanunuliwa na kampuni hiyo.
"China ni soko nambari moja duniani kwa pilipili, kwa hivyo ni muhimu sana kwetu," Uwizeyimana amesema. "Tuna matumaini ya mauzo ya nje imara na ya juu zaidi kwenda China."

Ndege wa Kwarara waingia msimu wa kuzaliana huko Shaanxi, China

Eneo la kaboni-sifuri katika Mkoa wa Hainan laonyesha vitendo vya kijani vya China

Vifaa vya kisasa vya usafi vyatoa huduma kwenye Mkutano wa Mwaka wa Jukwaa la Boao la Asia 2026

Eneo Jipya la Xiong'an la China labadilika kuwa mji wenye nguvu hai kutoka mpango
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
