Wakulima wa chai waleta harufu nzuri kutoka milimani kwa wateja wa mijini mkoani Anhui (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 28, 2026
Wakulima wa chai waleta harufu nzuri kutoka milimani kwa wateja wa mijini mkoani Anhui
Wachuma chai wakiondoka kwenye shamba la chai katika Kijiji cha Houkeng cha Eneo la Huangshan la Mji wa Huangshan, Mkoa wa Anhui, mashariki mwa China, Aprili 24, 2026. (Xinhua/Zhang Duan)

Taiping Houkui ni chai maarufu ya kijani ya Mkoa wa Anhui, mashariki mwa China, inayojulikana kwa majani yake bapa na marefu. Chai hiyo ina harufu yake kipekee ya maua na matunda, na ukiinywa utasikia ladha tamu kidogo. Hivi karibuni, eneo kuu la uzalishaji wa chai hiyo ya Taiping Houkui, shamba la chai lililoko kwenye milima mirefu katika Kijiji cha Houkeng cha eneo la Mji wa la Huangshan, limeingia kwenye msimu wa mavuno wenye pilika nyingi zaidi.

Ili kuchuma majani freshi ya chai kwa kutengeneza chai hiyo ya Taiping Houkui, wakulima wenyeji wa chai na wachumaji wa majani ya chai walioajiriwa wanatakiwa kupanda milima na kuvuka mito ili kufikia shamba la chai na kuanza kufanya kazi zao ndani ya misitu minene kwa kukabiliwa na ukungu wa asubuhi mapema.

Mwaka 2025, uzalishaji wa jumla wa chai wa Eneo hilo la Huangshan ulifikia tani 1,722.8, ambazo zilitimiza thamani ya jumla ya uzalishaji ya yuan bilioni 3.9 (dola za Marekani karibu milioni 571).

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha