Lugha Nyingine
Utamaduni wa jadi wa China waonekana kwa mara ya kwanza kwenye sherehe za Siku ya Uhuru wa Togo (2)
![]() |
| Wanajeshi wakishiriki kwenye gwaride la Siku ya Uhuru wa Togo, Lome, Togo, Aprili 27, 2026. (Xinhua/Si Yuan) |
LOME - Togo Jumatatu ilifanya gwaride kubwa la kijeshi na maandamano ya raia kusherehekea miaka 66 tangu kupata uhuru wake.
Rais wa Togo Jean-Lucien Savi de Tove, Rais wa Baraza la Mawaziri Faure Gnassingbe, pamoja na viongozi wengine, wawakilishi kutoka sekta mbalimbali na wajumbe wa kundi la wanadiplomasia, walihudhuria hafla hiyo.
Balozi wa China nchini Togo Wang Min alialikwa kushuhudia sherehe hiyo kutoka kwenye jukwaa kuu.
Sherehe ya mwaka huu ilifanyika chini ya kaulimbiu ya: "Ukarimu na Upatanishi katika Huduma ya Diplomasia Hai kwa Amani, Usalama na Maendeleo ya Kijamii na Kiuchumi ya Mataifa."
Kundi la utamaduni wa jadi wa China linaloundwa na wanafunzi kutoka Taasisi ya Confucius katika Chuo Kikuu cha Lome limeonekana kwa mara ya kwanza kama kundi la kwanza la utamaduni wa jadi katika gwaride hilo, ikiwa ni mara ya kwanza kwa kundi la utamaduni wa kigeni kushiriki katika historia ya gwaride la Siku ya Uhuru wa Togo.
Jumla ya wanafunzi 34 wa Taasisi hiyo ya Confucius, wakiwa wamevalia mavazi ya kijadi ya Hanfu na ya kikabila, walikuwa wameshikilia miavuli yenye mapambo ya peoni, huku wachezaji wa ngoma za dragoni na simba wakitembea katikati yao.
Onyesho hilo liliwasilisha salamu za dhati za sherehe kwa watu wa Togo na kupata makofi ya shangwe na sifa kubwa kutoka kwa hadhira.
Balozi wa China Wang ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua kwamba uwepo wa "rangi nyekundu ya China" umejitokeza katika gwaride hilo, ukienda sambamba na maonyesho ya utamaduni wa jadi wa Togo na kwa pamoja kuchora picha dhahiri ya mawasiliano yenye maelewano kati ya ustaarabu wa China na Togo.
Ameongeza kuwa onyesho hilo limekuwa moja ya matukio ya Mwaka wa Mawasiliano kati ya watu wa China na Afrika.

Ndege wa Kwarara waingia msimu wa kuzaliana huko Shaanxi, China

Eneo la kaboni-sifuri katika Mkoa wa Hainan laonyesha vitendo vya kijani vya China

Vifaa vya kisasa vya usafi vyatoa huduma kwenye Mkutano wa Mwaka wa Jukwaa la Boao la Asia 2026

Eneo Jipya la Xiong'an la China labadilika kuwa mji wenye nguvu hai kutoka mpango
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
