Lugha Nyingine
Droni zasafirisha miche ya miti katika bustani moja mjini Lanzhou, Gansu, China (2)
(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 29, 2026
![]() |
| Droni ikisafirisha miche ya miti katika bustani moja mjini Lanzhou, Mkoa wa Gansu, kaskazini magharibi mwa China, Aprili 27, 2026. (Xinhua/Lang Bingbing) |
Katika siku chache zilizopita, droni kadhaa zimekuwa zikipishana kwenda na kurudi kwenye vilima vilivyotelekezwa vyenye eneo la ukubwa wa hekta 153 hivi katika sehemu ya Mji wa Lanzhou, Mkoa wa Gansu, kaskazini magharibi mwa China ili kuinua miche kwa usahihi na kusaidia kwa ufanisi shughuli za upandaji miti.
Ofisi ya maliasili na mipango ya mji huo imesema kwamba ikilinganishwa na ufanyaji kazi wa kawaida wa kutumia nguvu kazi, droni hizo zimekuwa zenye kufaa zaidi kwa maeneo yenye mazingira magumu, ni salama zaidi na zenye kuokoa muda zaidi kwa kusafirisha miche ya miti.
(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




