Lugha Nyingine
Safari za abiria wa reli za China zazidi milioni 100 wakati wa mapumziko ya Siku ya Mei Mosi (2)
![]() |
| Abiria wakionekana kwenye jukwaa katika Stesheni ya Reli ya Huaibei, Mkoa wa Anhui, mashariki mwa China, Mei 5, 2026. (Picha na Wan Shanchao/Xinhua) |
BEIJING - Safari za abiria kwenye njia za reli nchini China zimezidi milioni 100 wakati wa mapumziko ya siku 5 ya Mei Mosi ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyokwisha jana Jumanne, kampuni ya kundi la kitaifa la reli la China imesema katika taarifa yake ya jana Jumanne.
Takwimu zilizotolewa na kampuni hiyo zimeonesha kuwa, mfumo wa reli nchini China umefanya kazi kwa usalama na kwa utaratibu mzuri wakati wa siku hizo za mapumziko, ambapo safari za abiria kwenye njia za reli zikifikia milioni 117 hadi juzi Jumatatu.
Kampuni hiyo imesema kuwa, njia za reli kote nchini China zimesafirisha abiria zaidi ya milioni 20.38 siku ya Jumatatu pekee iliyopita. Na idadi ya abiria waliorudi nyumbani baada ya usafiri iliongezeka zaidi jana Jumanne, abiria waliokadiriwa kupanda treni walifikia milioni 23,hivyo kampuni ya reli iliongeza treni 2,225 za ziada kwa huduma za siku hiyo ya Jumanne.
Kwa mujibu wa takwimu za tiketi kutoka kwenye jukwaa rasmi la kununulia tiketi za usafiri wa reli, maeneo yaliyokuwa na wasafiri wengi zaidi siku hiyo ya Jumanne ni pamoja na Beijing, Guangzhou, Shanghai, Chengdu na Shenzhen.
Mamlaka za reli zimekuwa zikihamasisha rasilimali za uwezo ili kusimamia pilika za safari za kurudi nyumbani na kuhakikisha abiria wanasafiri salama na kwa utaratibu mzuri. Kwa mfano, treni 707 za ziada zinazohudumia njia zenye kupendelewa na abiria wengi zilikuwa zimepangwa katika Mkoa wa Guangdong, kusini mwa China.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




