Lugha Nyingine
Matumizi ya kibiashara ya AI yaongezeka kwa kasi kubwa kote China
![]() |
| Mwanamke akitembelea maonyesho ya kudumu kwenye Kituo cha Maonyesho cha Zhongguancun cha Beijing, Machi 25, 2026. (Xinhua/Ju Huanzong) |
BEIJING - Teknolojia ya AI ni mwakilishi wa nguvukazi mpya za uzalishaji zenye sifa bora na alama ya kipekee katika maendeleo ya sayansi na teknolojia ya China, hivi sasa teknolojia hiyo inasukuma mbele maendeleo ya kupanda ngazi ya juu na kufanya uvumbuzi katika sekta mbalimbali nchini China.
Ripoti ya kazi ya serikali ya China ya mwaka huu imesema kuwa, ni lazima kuharakisha matumizi ya vituo vya AI vya kizazi kipya na mbadala wa AI, kuhimiza matumizi makubwa ya kibiashara ya AI katika sekta na nyanja muhimu, na kuandaa shughuli za aina mpya na za mfano wa aina mpya katika shughuli asili za AI.
Kadiri China inavyopiga hatua madhubuti kwa kusukuma mbele maendeleo ya sifa bora, soko lake kubwa na mfumo wa viwanda ulioimarishwa vizuri vinaleta uwezekano mkubwa kwa matumizi ya AI katika siku za baadaye.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




