Lugha Nyingine
Wizara ya Mambo ya Nje ya China yasema nguvu ya ushindani ya kampuni za China haitokani na ruzuku
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Mao Ning, alipojibu maswali Juni 3 kwenye mkutano na wanahabari amesema kuwa nguvu ya ushindani ya kampuni za China haitokani na ruzuku.
Habari zimesema kuwa, Shirika la Ushirikiano wa Uchumi na Maendeleo (OECD) lilitoa ripoti likisema kuwa, katika nyanja 15 muhimu za viwanda ikiwemo magari, uundaji wa meli na nishati ya jua, asilimia 60 ya ongezeko la soko kwa kampuni za China limetokana na ruzuku tangu mwaka 2005. Katibu mkuu wa shirika hilo amesema, utoaji mkubwa na endelevu wa ruzuku kwa viwanda umevuruga soko la dunia, na kuonesha nguvu ya ushindani usio wa haki na kusababisha hali ya uzalishaji kuzidi mahitaji ya soko.
Akizungumzia suala hilo, msemaji huyo wa China amesema, nguvu ya ushindani ya kampuni za China haitokani na ruzuku, bali inatokana na ushindani kamili wa sokoni, uvumbuzi endelevu wa teknolojia, mpangilio wa kampuni hizo kwa mtazamo wa dunia, pamoja na faida za soko kubwa. Sera ya China ya utoaji ruzuku inafuata kwa makini kanuni za Shirika la Biashara Duniani (WTO). Amelitaka shirika husika la kimataifa lifanye kazi ya kiujenzi, na wala sio kinyume chake.

Meli kubwa ya kitalii ya pili kuundwa ndani ya China yakamilisha jaribio la kwanza la baharini

Hifadhi ya Taifa ya Kruger ya Afrika Kusini yaadhimisha miaka 100

Nishati ya kijani yahimiza maendeleo yenye sifa bora katika Mkoa wa Xizang, China

Madaraja ya matao yenye mapaa ya mbao yahifadhiwa vizuri katika Mkoa wa Fujian, China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma